SIMBA WATOA TAMKO LAO BAADA YA MANJI KUREJEA YANGA
Simba wamesisitiza kwamba hawahofii kitendo cha Yusuf Manji kurejea Yanga kama mwenyekiti na kwamba hawezi kuathiri kwa vyovyote mipangilio yao.
Manji alitangaza Jumapili iliyopita kurejea Yanga na mzuka wake uliwapa wachezaji nguvu ya kuwapiga USM Algiers mabao 2-1 kwenye mechi ya Shirikisho.
Tathmini inaonyesha kwamba uwepo wa Manji Yanga kutaibua upinzani mkubwa miongoni mwa timu hizo mbili kongwe kwenye kutokana na Simba kuwa na kiburi cha muwekezaji, Mohammed Dewji ‘MO’.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully alisema kuwa, wao hawamhofii Manji na badala yake wanapambana kuona timu yao inafanya vyema msimu huu.
“Sisi hatuna upinzani na Manji bali tuna upinzani na Yanga na hatujali uwepo wake na badala yake tutapambana kuhakikisha tunafanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu.”
Simba ndiyo klabu iliyosajili wachezaji ghali zaidi msimu huu tofauti na klabu zingine zinazoshiriki ligi hiyo ambayo inaanza leo bila mdhamini mkuu.
Hivi uwa unawahoji hao viongozi au unaandika tu kwa utashi wako ili kupendezesha habari
ReplyDeleteNilishasemaaa hawa niwachambuziii uchwaraaa.
ReplyDeleteAnaandika andikaa tuuu hamna cha kuhoji