MARTIAL, HAZARD, MINA, LOOKMAN: TETESI KUBWA ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMATANO
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amemuomba naibu mwenyekiti mtendaji wa klabu hiyo Ed Woodward kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa anayechezea klabu hiyo Anthony Martial, 22. (Star)
Lakini Martial ameamua kwamba anataka kusalia Old Trafford na anataka kupigania nafasi yake katika kikosi cha Mourinho. (Sun)
Real Madrid wanatarajiwa kuwasilisha ofa yao ya mwisho ya kutaka kumnunua nyota wa Chelsea raia wa Ubelgiji Eden Hazard, 27, kabla ya dirisha kuu la kuhama wachezaji Ulaya kufungwa mwishoni mwa mwezi huu. (Mirror)
Barcelona wanaweza wakamnunua tena beki wa Colombia Yerry Mina kutoka Everton kwa euro 60m (£53.83m) baada ya kumuuza mchezaji huyo wa miaka 23 kwa Everton kwa euro 30.25m (£27.19m) siku ya mwisho ya kuhama wachezaji England, lakini hawawezi kutumia fursa hiyo kwenye kifungu cha mkataba wa kuhama kwake hadi mwaka 2020. (Marca)
Manchester City wataamua iwapo watamwita tena kipa wao mwenye miaka 19 Aro Muric aliye NAC Breda kwa mkopo baada ya uchunguzi zaidi wa kimatibabu kubaini kwamba kipa wao wa akiba Claudio Bravo aliumia kwenye kano za kifundo cha mguu akifanya mazoezi Alhamisi. (Telegraph)
Hata hivyo klabu hiyo ya Uholanzi haitarajii mchezaji huyo anayechezea timu ya taifa ya wachezaji wa chini ya miaka 21 ya Montenegro achukuliwe tena na klabu hiyo ya Etihad. (Manchester Evening News)
West Ham wanamtafutia kiungo wa kati mwenye miaka 19 Reece Oxford klabu nyingine ya kumchukua kwa mkopo. Msimu uliopita, alikuwa an klabu ya Ujerumani ya Borussia Monchengladbach kwa mkopo. (Mail)
Arsenal wamekataa kukubali ombi la kiungo wa kati Aaron Ramsey la kutaka aongezewe ujira wake mara mbili lakini wana matumaini makubwa kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales mwenye miaka 27 atatia saini mkataba mpya. (Evening Standard)
Mahasimu wa jadi Real Madrid na Atletico Madrid wote wanammezea mate beki wa kati wa Chelsea Marcos Alonso, 27, na wanataka kumchukua kabla ya soko kufungwa Ulaya mwezi huu. (AS)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment