STRAIKA HATARI YANGA ATUMA SALAAM ZA KUTISHA KWA OKWI LIGI KUU
Straika mpya wa Yanga , Heritier Makambo aliyesajiliwa kutoka FC Lupopo ya Congo, amesema kuwa matarajio yake ni kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu ujao, imeelezwa.
Makambo ambaye alisajiliwa na Yanga kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili ameeleza kuwa lengo kubwa ambalo amekuja kuifanyia Yanga ni kucheka na nyavu pekee.
Makambo amesema kwa sasa anazidi kujifua na wenzake huko Morogoro ambapo kikosi kimeweka kambi ya wiki mbili ili msimu utakapoanza aanze kutema cheche zake kuwaonesha Yanga kuwa kazi yake si nyembamba.
Kauli ya Makambo inaonesha dhahiri shahiri kuwa anataka kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye ametwa tunzo ya mfungaji bora kwa msimu uliopita akifunga mabao 20.
Wakati Makambo akitaka kumpiga chini Okwi, straika huyo yuko nchini Uturuki hivi sasa akijinoa na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya tamasha la Simaba Day na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Kichwa cha habari mbona kiko mbali kabisa na habari uliyoiandika , IPI HATARI YA STIKER huyu, IPI habari ya KUTISHA hapo kwa hakika Sana'a ya uandishi bado no tatizo kwako😶😶
ReplyDeleteHuyo aliekuja kwa meno ya juu kweli anamjuwa Okwi au kafundushwa kuropokwa hayo? Kwanza angebidi aelezwe kiukweli yaliyojiri yanga hata ikafika hadi ya kukimbiwa na kocha Lindumina, kukimbiwa na mfadhili, kugoma na kukimbiwa kwa wachezaji nyota na kujiuzulu kiongozi hadi kiongozi kulipopelekea kupoteza mataji yote na kufungwa kila mechi wanayocheza na ndio baadae kutowa hayo majigambo yasio na mana
ReplyDeleteMnatuletea yaleyale ya msimu ule aliposajiliwa mchezaji fulani pale Yanga mkamuita WINGA TELEZA kumbe hamna kitu, akafukuzwa baada ya mwezi mmoja tu. Mpira uwanjani, sio magazetini.
ReplyDelete