August 3, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Simba leo kinashuka tena dimbani katika Uwanja wa Kartepe jijini Instambul, Uturuki kucheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Ittihad Riadhi De Tanger ambayo ni bingwa mtetezi huko Morocco.

Simba watakuwa wanapiga kibarua cha pili baada ya kile cha kwanza dhidi ya Mouolodia kwenda sare ya bao 1-1 huku mechi ikikatishwa na mvua kubwa ambayo ilinyesha mnamo dakika ya 65 kipindi cha pili.

Simba watacheza na klabu ya Tanger ambayo pia inashiriki Ligi Kuu Morocco ili kuzidi kukipa maandalizi kikosi chake kwa ajili ya tamasha la Simba Day ambalo watacheza dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana Agosti 8 mwaka huu.

Baada ya kukamilisha kambi ambayo ni ya wiki mbili huko Uturuki, Simba wataanza safari ya kurejea nchini Agosti 4 tayari kabisa kwa maandalizi ya mwisho kuelekea tamasha hilo pamoja na msimu mpya wa ligi.


3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic