August 22, 2018


Na George Mganga

Wakati Simba wakitamba kuanza na ushindi katika harakati za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara leo, uongozi wa klabu ya Tanzania Prisons umewataka wajiandae haswaa.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Prisons, Anvintishi Abdallah, amesema kuwa wao wameshajiandaa kikamilifu kwa ajili ya mchezo huo utaokuwa wa kwanza kwao msimu hu.

Abdallah amewaahidi Simba kujiandaa vema kwani watakuja na moto wenye balaa la aina yake na ikiwezekana alama tatu zikaelekea jijini Mbeya.

Tayati Prisons walishawasili jijini Dar es Salaam wakiwa na siku kadhaa kwa ajili ya kipute hicho kitakachopigwa majira ya saa 1 kwenye Uwanja wa Taifa.


Wakati Simba wakianza kukupiga na Prisons leo, watani zao wa jadi wataanz mbio hizo za ubingwa kesho kwenye Uwanja huohuo kuwakaribisha Mtibwa Sugar FC ya Morogoro.

3 COMMENTS:

  1. Kutishwa na hivi vi timu vidogo vidogo wamejitakia wenyewe Simba. Soka waliocheza katika mechi yao dhidi ya Mtibwa ilikuwa ya ovyo kabisa. Mechi ya leo wachezaji wajitume. Furaha yao ya mishahara mikubwa ioneshwe uwanjani. Watu wanataka ushindi mkubwa, sio kuruka ruka tu uwanjani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. SIMBA TUNATAKA MAGOLI SISI. MPIRA WA PASI MIA BILA MAGOLI HATUTAKI.

      Delete
    2. This comment has been removed by the author.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic