KESSY AFUNGUKA MAZITO YA MOYONI BAADA YA KUITWA NA AMUNIKE TAIFA STARS
Beki Mtanzania anayekipiga katika klabu ya Nkana Red Devils ya Zambia, Hassan Kessy, amefurahishwa na kitendo cha Kocha mpya wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike kumuita katika kikosi hicho.
Amunike ametangaza jana kikosi cha Stars ambacho kitavaana na timu ya taifa ya Uganda katika mchezo wa kuwania kucheza AFCON Septemba 8 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku jina la Kessy likiwa ndani.
Kessy ameeleza kuwa ataonesha kile ambacho anacho akiwa kama mchezaji ambaye amebahatika kucheza soka la kimataifa ndani ya Afrika.
Beki huyo ambaye alijiunga na Nkana akitokea Yanga kama mchezaji huru, ameahidi kumpa ushirikiano mzuri Amunike ili waweze kumridhisha ndani ya Uwanja kwa maana ni mgeni wa soka la Tanzania.
Aidha, Kessy anaamini taifa litazidi kuwapa sapoti kubwa kama timu ili waweze kufanya vizuri zaidi katika harakati za kulikuza soka la Tanzania kwa maana bado linapitiwa na changamoto nyingi.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteHongera Sana mdogo wangu hakika mungu ndie mkombozi Wako sababu kila wanapokucheka unapojaribu kuchechemea mungu ukuinua na kukushika mkono na kukuinyesha njia sahihi aibu kwao wanaotamani uanguke wakucheke sura zimewapaka wakubwa wazima waliokosa haya
ReplyDeleteNdio kukua huko maana aliondoka simba baada ya kuwasaliti uwanjani akaenda yanga kule kakutana na somo la kuachwa dakika za mwisho kwenye usajili kwakweli ana bahati kupata nafasi ya kucheza ligi mwaka huu
Delete