August 3, 2018


Baada ya aliyekuwa Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' kustaafu rasmi soka la ushindani, uongozi wa klabu hiyo umemtangaza Kelvin Yondani kuwa mbdala wake.

Yondani amechukua rasmi kitambaa cha unahodha ndani ya kikosi cha Yanga ambacho alikuwa akikikivaa kama msaidizi ukiachana na Cannavaro ambaye alikuwa Nahodha mkuu.

Kutoka na kustaafu kwa Cannavaro, uongozi Yanga umekabidhi rasmi Yondani kitambaa cha unahodha huo huku atakuwa akisaidiwa na kiungo, Thaban Kamusoko pamoja na beki, Juma Abdul.

Kikosi hicho kipo mjini Morogoro hivi sasa kikijiandaa na mchezo dhidi ya USM Alger na msimu mpya wa ligi unaotarajia kuanza Agosti 22 mwaka huu.

Yanga waliwasili Morogoro jana kwa kambi maalum ya wiki mbili kujiandaa na mchezo dhidi ya Waarabu hao ambao ni wa Kombe la Shirikisho Afrika pia kuelekea Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic