September 26, 2018


Katika hali ya kushangaza, Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga amesema kikosi chake kimekuwa kikicheza na wanaume ndani ya dakika 90 na si wanawake, hali inayopelekea wachezaji wake kukosa nguvu kipindi cha pili.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya kuibuka hoja na malalamiko kwa baadhi ya mshabiki wa Yanga wakihoji inakuwaje timu imalize nguvu kipindi cha pili.

Katika michezo yote ya msimu huu wachezaji wa Yanga wamekuwa wakikata pumzi haswa baada ya dakika kadhaa kuanza kwa kipindi cha pili na kuepelekea maswali kwa timu na Kocha kwa ujumla.

Kuwepo kwa mjadala huo kumemfanya Zahera aibuke na kueleza kuwa wamekuwa wakicheza dhidi ya wanaume wenzao ambao wamekuwa wakija juu kwa ajili ya kupata matokeo.

Zahera amesema kama ingekuwa ni wanawake pekee basi wasingeweza kuwakatisha pumzi wachezaji na akieleza kuwa hilo ni jambo la kawaida kwa wachezaji.

3 COMMENTS:

  1. Hivi kocha haeleweki akielezea jambo ? Au umeamua kupotosha.

    Uzuri alichosema kipo kwenye mtandao rudia kumsikiliza kama lengo lako ni ukweli.

    ReplyDelete
  2. Hivi kocha haeleweki akielezea jambo ? Au umeamua kupotosha.

    Uzuri alichosema kipo kwenye mtandao rudia kumsikiliza kama lengo lako ni ukweli.

    ReplyDelete
  3. mie wasiwasi wangu uko ktk baadhi ya timu kuwa wachezaji wao wanatumia madawa ya kuongenza nguvu.TFF kuweni makini ktk suala hili baada ya mechi pimeni wachezaji hata sita ili kuwe na fair play

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic