September 18, 2018


Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi kutoka nchini Mali kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 kati ya Cape Verde na Tanzania katika Uwanja wa Estadio National  Oktoba 12,2018.

Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Boubou Traore akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Drissa Kamory Niabe, Mwamuzi msaidizi namba 2 Baba Yomboliba na Mwamuzi wa akiba Gaoussou Kane na Kamishna wa Mchezo anatokea G. Equatorial Tadeo Nsue Onva.

Aidha mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa 
Oktoba 16, 2018 Kwenye Uwanja wa Taifa wenyewe 
utachezeshwa na Waamuzi kutoka Djibouti

Mwamuzi wa katikati atakuwa Souleiman Ahmed Djama, 
na Mwamuzi msaidizi namba 1 Farhan Bogoreh Salime, Mwamuzi msaidizi namba 2 Rachid Waiss Bouraleh na Mwamuzi wa akiba Bilal Abdallah Ismael.

Kamishna wa mchezo anatokea Malawi Maxwell Mtonga, Mtathmini waamuzi anatokea Rwanda Michael Gasingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic