Inaelezwa kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefikia makubaliano ya kuachana na Kocha Emmanuel Amunike aliyekuwa anainoa Taifa Stars.
Hatua hiyo imekuja kufuatia kuboronga mechi za mashindano ya AFCON yanayoendelea Misri.
Taarifa za ndani zinasema TFF hivi sasa ipo kwenye mchakato wa kumpata Mwalimu mbadala wa muda atakayeinoa Stars kuelekea michuano ya CHAN.
Hapo sawa ingawa TFF wamechelewa sana kufanya maamuzi haya kwani Amunike ilitakiwa atimuliwe mapema tu hata kabla timu haijaenda AFCON. Atafutwe kocha mwenye uzoefu mkubwa na mwenye hadhi ya kufundisha timu ya Taifa, pia asiwe mzalendo.
ReplyDeleteTFF wamechelewa kumtimuwa Amunike ilikuwa baada ya kufungwa na Lethoso tu ila yaliyopita iwe darasa kwetu sote.Mpira ni serious business yenye ushindani wa hali ya juu. Sio tena kazi ya kuichukulia kimzaha mzaha. Na kama tunataka kuwa washindani wa kweli kwenye mpira basi lazima tujipange.Lakini kati ya biashara na mfanya biashara vyote vinaumuhimu wake ila unaweza kuwa na mlima wa dhahabu lakini kama kutakosekana wafanya biashara mahiri basi si ajabu dhahabu hiyo ikapotelea hivi hivi tu na isilete impact yeyote ile ya maisha kuwa bora kwenye jamii inayowazunguka. Hii ni sawa kabisa na kwenye mpira tunaweza tukawa na mlima wa vijana wenye vipaji chungu tele lakini ukosefu wa wataalam wa uhakika wa kuwaendeleza ili kuviimarisha vipaji vyao na kuwa wachezaji kamilli likawa tatizo. Na hapa ndipo Suala la kocha mtaalam na mzoefu hasa yule wa kukuza vipaji linapokuja kuwa muhimu kabisa kwa nchi kama yetu Tanzania. Tunahitaji kocha au makocha wenye ujuzi wa ngazi za kimataifa ili kutujengea misingi imara ndani ya timu yetu ya Taifa. Hata zahera wa Yanga awe miongoni mwa makocha wanaofikiriwa kupewa majukumu ya kuinoa Taifa stars .
ReplyDeleteUamuzi wa Busara tutafanikiwa siyo kuwa na kamanda asiyejua ubora wa silaha zake wakati anaenda vitani,vitani si sehemu sahihi ya kujaribisha silaha kama alivyo kuwa anafanya Amunike, ni utani na masihara yaliyokubuhu aidha kwa kutuona Watanzania ni mbumbu hatuoni wala hatujui.Asanteni sana kwa uamuzi mzuru.
ReplyDeleteHakuna haki,haki itatendeka kma na TFF no watajiuzulu
ReplyDeleteHata raisi wa chama cha mpira cha Nigeria kaishangaa Tanzania kumkabidhi Amunike ukocha wa timu yetu ya Taifa.TFF wanapaswa kujiuzulu mchana kweupe..Na kama Takukuru hawatakwenda kufuuatilia skendo ya Amunike basi nitashangaa sana kwani kuna upotevu mkubwa wa malengo pamoja na mali uliosababiswa na uzembe wa TFF kuajiri kocha wa chini ya kiwango. Aidha uteuzi wa Amunike haukuwa wa wazi na kiushindani kwa makocha wangine nao wakapata nafasi ya kufungua tenda ya maombi ya kandarasi ya kazi. Uamuzi wa TFF ulikuwa wa kumpendelea kumpa Amunike kazi moja kwa mojw bila ya ushindani wowote sidhani kama ni sahihi kwa hivyo tunaomba Takukuru kuichunguza ajira ya Amunike ndani ya TFF na kwa kigezo gani kilimfanya awe mstahiki pekee wa ajira kwa timu yetu ya Taifa?
ReplyDeleteKocha gani tokea mwanzo wa game hadi mwisho amekaa tu hatoi maelekezo, yaani akipanga kikosi kamaliza. Eti nidhamu c aende akafundishe OMISHUMTA na Wallace Karia ajiuzuru pia maana amefeli sehemu kubwa hata kwenye ligi ya ndani.
ReplyDeleteKim Paulsen
ReplyDeleteTFF waige mfano wa shirikisho la soka la misri,ili tupate wengine wanaoweza kua na Maono ya kusogea zaidi ya hapa tulipofika
ReplyDeleteKama tff haitabadilika basi itakuwa kazi ni bure tu kwani viongozi wote waliopo wamethibitisha kuwa wamekosa sifa za kuongoza kandanda wanatakiwa wajiuzulu wao kwanza Ligi mbovu imekosa hata msisimko haina hata wafadhili kwa ufupi ikiwa shirikisho ni bovu hata timu yenu ya Taifa nayo huwa mbovu piamsitafute sababu.
ReplyDeleteNatupa karata yangu kwa makocha HANS PLUIJM na KIM POULSEN au BONIPHACE MKWASA kwani hawa wote wanawajua wachezaji wetu wa Tanzania na pia mazingara wameshayazoea.
ReplyDeletehuyo mkwasa si ndio alikuwa kocha wakati tunafungwa saba na waaligeria au umesahau
DeleteUamuzi upo sahihi. Mbadala wake apewe Kim Paulsen, alishawahi kuhoji hata Ismail Rage juu ya kilichopelekea kuindolewa kwa coach huyo wakati alionekana kufanya vizuri na timu ya taifa. Kim Paulsen aliondolewa wakati huo timu ilikuwa ina perform na kucheza vizuri tena kitim.
ReplyDeleteIkishindikana kwa Kim basi apewe etiene wa Azam awekocha wakudumu
ReplyDeleteKama timu ya taifa ni kama kichwa cha mwendawazimu kila mtu ajifunzia turudisheni makocha walioboronga!. Misri wamepiga chini kocha na rais wa shirikisho naye amewajibika. Vipi hapa bongo tunabembeleza?
ReplyDeleteAtafutwe kocha mwenye uwezo wa kweli na hata akisema apewe muda watu wawe na imani nae.
ReplyDeleteKama TTF wasikivu basi babu wa stand united mfaransa aliewahi kuifundisha Simba pia. Ni kocha mzuri kabisa wa kutujengea timu yenye nidhamu na ni mtaalamu wa soka la vijana vile vile .
ReplyDeletemi naona wachezaji hawajitumi kabixa kwan wamepita makocha zaidi ya kumi na kila kocha anamfumo wake na wachezaji wake hivyo hata kuendelea kwa taifa ni ngumu xana
ReplyDelete