Kikosi cha Taifa Stars kimeondoka leo
alfajiri kwenda Windhoek, Namibia kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya wenyeji itakayochezwa Machi 5
mwaka huu.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager ina msafara wa watu 25 unaoongozwa na mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Timu
imefikia hoteli ya Safari jijini humo.
Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa
Sam Nujoma, na kikosi cha Taifa Stars kipo chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi
wa TFF, Salum Madadi ambaye ana leseni A ya ukocha inayotambuliwa na Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Namibia (Brave Warriors)
inayofundishwa na kocha Ricardo Mannetti imeingia kambini jana (Machi 2 mwaka
huu) kwa ajili ya mechi hiyo ambayo tiketi zake zilianza kuuzwa Februari 28
mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment