September 30, 2018


Hatimaye ile siku ya furaha, huzuni na machozi kwa mashabiki na wapenzi wa soka nchini imewadia ambapo vigogo wawili wenye historia kubwa ya kandanda watakapopambana hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ukiachana na maandalizi ya timu hizo tangu wiki iliyopita mpaka sasa, kuna vita inayoendelea nje ya uwanja kutoka kwa maafisa Habari wa timu hizo, Haji Manara kwa upande wa Simba na Dismas Ten wa Yanga.

Vita hiyo imekuwa ikiendelea katika mitandao ya kijamii hasa kwenye mtandao wa Istagram ambapo kila mmoja akijaribu kutupa vijembe hewani katika kuhamasisha mashabiki na wapenzi wa timu yake waamini kuwa wanao uwezo wa kuibuka na ushindi dhidi ya mpinzani wake katika mchezo huo.

Haji Manara katika ukurasa wake wa Instagram amekuwa akiandika ujumbe mwingi unaowalenga mahasimu wake Yanga huku akijitetea kuwa anafanya hivyo ili kuongeza ladha ya ushindani halisi baina ya timu hizo. Mfano katika ujumbe wake wa leo kuelekea mchezo huo, ameandika,

” Nawakumbusha tu kama kuna mchezaji kajiandaa kutema mate tena mtuambie mapema tuje na makopo maana tunawajua “, ujumbe uliowalenga wachezaji wa Yanga.

Naye Afisa Habari wa Yanga kwa upande wake hayupo nyuma katika kujibu mapigo ya Haji Manara, amekuwa akituma ujumbe mbalimbali wenye kuwaamsha mashabiki wa timu yake kuwa wanao uwezo wa kushinda mchezo huo.

Ujumbe wake wa mwisho kuelekea mchezo huo, Dismas Ten ameweka matokeo ya ‘1-4’ akimaanisha kuwa Yanga itaibuka na ushindi wa mabao manne kwa moja hii leo.

Simba na Yanga zinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu, mchezo ambao endapo Simba ikishinda itafikisha alama 13 na kukwea hadi nafasi ya pili ya msimamo nyuma ya kinara Mbao Fc kwa alama moja. Yanga ikifanikiwa kushinda itafikisha alama 15 na kuongoza ligi mbele ya alama moja dhidi ya Mbao Fc yenye alama 14 mpaka sasa.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic