September 22, 2018


Kocha mwenye maneno mengi pengine kuliko wote nchini, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ameibuka na kueleza kuwa uwepo wa Masoud Djuma kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Mbao usingesababisha timu hiyo kushinda.

Julio amefunguka kwa kusema katika mpira wa miguu huwa kuna matokeo ya aina tatu ambayo yanatokea kulingana na maandalizi ya timu husika ndani ya uwanja.

Kocha huyo wa Dodoma FC, ameeleza hayo baada ya mashabiki wengi kuanza kuutupia lawama uongozi kuwa kitendo cha kumuengua Djuma na kumuacha Dar es Salaam bila kuambata naye mikoani kumesababisha Simba isivune pointi tatu.

Katika mchezo huo uliopigwa Alhamis ya wiki hii, Simba ilipoteza kwa bao 1-0 na kupoteza alama zote tatu huku mchezo wa nyuma yake ikitoka suluhu bila kufungana na Ndanda FC,

Ratiba ya ligi inaonesha Simba itakuwa tena na kibarua kingine Shinyanga kucheza na Mwadui FC kwenye uwanja wa CCM Kambarage.

3 COMMENTS:

  1. Ahsante Julio,waeleze hawa mambumbumbu wasiojuo soka,madaraka kaeleza vyema wanambeza

    ReplyDelete
  2. Kichwa cha habari ni tofauti na habari yenyewe,hii blog itabidi tuishtaki kwa Ninja Kangi Lugola aichukulie hatua kwa habari za upotoshaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic