September 22, 2018


Kutokana na klabu ya Singida United kukabiliwa na ukata wa fedha, imeelezwa kuwa nyota wake wa kimataifa kutoka Uganda, kiungo Shafik Batambuze, ameanza mazungumzo na Gor Mahia FC ya Kenya.

Taarifa hizo zimekuja kufuatia mchezaji huyo kuelezwa kuwa anaidai fedha za mshahara klabu hiyo yenye maskani yake mjini Singida.

Batambuze mpaka sasa hajacheza mchezo wowote ndani ya timu huyo tangu kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu Bara 2018/19.

Singida imekuwa kwenye mpasuko hivi karibuni kwa baadhi ya waajiriwa wake kuanza kujiweka kando baada ya hali ya uchumi kuanza kuyumba.

Mbali na Batanbuze kugomea kucheza na sasa kuanza mazungumzo na Gor Mahia, makocha wake wasaidizi pia wameachia ngazi kwa sababu ya kutolipwa stahiki zao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic