September 19, 2018


Na George Mganga

Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda, amefunguka juu ya unazi wa mchezaji wake, Ali Kiba kuelekea mechi ya leo dhidi ya Coastal Union.

Yanga na Coastal Union zitakuwa na kibarua kizito leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo mechi itaanza majira ya saa 1 za usiku.

Mgunda ameeleza kuwa licha ya Kiba kuwa na mahaba na Yanga hadhani kama anaweza akaisaliti timu yake kwa kuwa yupo pale kikazi.

Kocha amesema hana hofu na Kiba kuipenda Yanga kwakuwa amemsajili kama mtumishi wa Coastal Union na lazima atimize wajibu wake kama mchezaji.

"Sina hofu na unazi wa Kiba kwa Yanga, ni mtumishi wa Coastal Union hivyo anapaswa kuwajibika kama wachezaji wengine. Sina hofu juu yake" alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic