MAAGIZO YA MBELIGIJI SIMBA KWA MASOUD DJUMA HAYA HAPA
Kocha Mbelgiji wa Simba, Patrick Aussems, amefunguka juu ya maagizo aliyompa Msaidizi wake, Masoud Djuma kuhusiana na mechi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga itakayopigwa Septemba 30 2018.
Aussems ameeleza kuwa Djuma alibakia jijini Dar es Salaam kuitazama Yanga ikicheza na Coastal Union ili kujua mbinu za kuimaliza kiulaini kuelekea mechi dhidi yao.
Mbelgiji huyo ambaye alishindwa kutamba mbele ya Mbao kwa kuambulia kichapo cha bao 1-0 amefunguka kumwacha Djuma Dar es Salaam kwa sababu anaifahamu Yanga vizuri kitu ambacho kitaisaidia Simba kujiandaa vizuri.
Kuelekea mechi hiyo Simba hawatocheza mchezo wao dhidi ya Biashara United uliokuwa umepangwa kupigwa Septemba 27 na Yanga kucheza Septemba 26 dhidi ya JKT Tanzania ili kuzipa timu hizo nafasi ya kujiandaa vema.
Unamuacha Djuma aisome Yanga eti kwa kuwa wewe huijui. Kwani unaijua Mwadui, unaijua Ndanda, unaijua Mbao.
ReplyDeleteKwani Ligi kuu ni Yanga au timu ishirini. Habu huyu Mzuzu aache kutufanya malofa. Hakuna timu yoyote wala mchezaji yeyote anayemjua Tanzania zaidi ya Simba.
Masoud angefanyika msaada sana na sote tumeona Simba ilipocheza Mzuzu akiwa na Masoud na bila Masoud.
Kama mnafikiri mnataka kumuacha Masoud muacheni tu kwani mnaemlipa ni MO na uongozi wa Simba ila Juzi mmepigwa chupa za maji basi jiandae kukutana na hasira za mashabiki kama matokeo yataendelea hivi kwani viwango vya uvumilivu tunatofautiana
Visingizio vya ooooh eti wamepaki basi sijui roli hiyo ndio kazi iliyomleta Mwalimu na analipwa mshahara. Awe mnyumbulifu na kubadili mifumo kulingana na upepo wa mechi ilivyo ili timu upate matokeo. Msituletee habari ya umiriki wa mpira kwa asilimia kubwa. Mashabiki wanataka ushindi
UONGO MTUPU. JARIBU KUSHIRIKIANA NA MSAIDIZI WAKO. UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU MKUBWA.
ReplyDeleteKwani mbao ulikua unawajua maana umeenda bila ya msaaidizi wako
ReplyDeleteKwani mbao ulikua unawajua maana umeenda bila ya msaaidizi wako
ReplyDeleteUngebaki wewe mwalimu mkuu ili uweze kuisoma vizuri badala ya Djuma ambaye amecheza nayo mara zote. Masoud angekwenda Mtwara na Mwanza kisha Shinyanga, wewe usubiri mechi ya Yanga. Kwani wewe umesajiliwa kwa ajili ya Yanga, au kuutetea ubingwa tena?
ReplyDeleteMkuu ndio abaki ili azisome timu kama kweli yeye no mwalim mkuu!
ReplyDelete