September 26, 2018


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa halitoruhusu ubabe wowote kwa wanaojiita makomandoo wa timu za Simba na Yanga kuelekea pambano lao kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Clifford Mario Ndimbo, amesema kwa sasa hakutakuwa na ubabe wowote utakaofanywa na makomandoo hao ndani ya uwanja kabla na baada ya mchezo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni mara baada ya makomandoo hao wa timu hizo kuwa sehemu ya kuharibu taratibu ikiwemo kuleta ubabe mbele ya waandishi wa habari baada ya mchezo kumalizika.

Ndimbo ameeleza kwa sasa wamewapiga STOP na badala yake hawatakuwa na utamaduni wao wa kuibukia Uwanjani ikiwemo sababu za kutaka kulinda Uwanja kabla ya mchezo, jambo ambalo si sahihi.

Maamuzi haya yamekuja ikiwa ni siku 4 pekee kuelekea mechi ya watani wa jadi itakayopigwa Septemba 30 2018 kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic