Kiungo mkabaji wa klabu ya Simba, Jonas MKude, ameungana na watanzania kuipa sapoti Taifa Stars ambayo inashuka dimbani huko Kampala Uganda kucheza na wenyeji The Cranes.
Stars inakipiga na The Cranes kuwania nafasi ya kufuzu kucheza AFCON 2019 kwenye Uwanja wa Mandele jijini humo majira ya saa 10 kamili jioni.
Kuelekea mechi hiyo, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mkude amewataka watanzania wote waungane kukiombea kikosi ili kiweze kufanya vizuri kwenye mechi hiyo.
"Sisi ni Tanzania. Sisi ni Taifa. Kwa pamoja tuungane kuwaombea wawakilishi wetu kwenye mchezo wa leo dhidi ya Uganda" ameandika.
Stars inacheza na Uganda ikiwa na alama moja pekee katika kund L sawa na Lesotho ambayo walitoka nayo sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati huohuo, Uganda inaongoza ikiwa na alama 3 baada ya kuifunga Cape Verde mechi ya kwanza kwa bao 1-0.









Taifa Stars ina nafasi ya kushinda zidi ya Uganda wasi wasi wangu mkubwa kwa Taifa Stars upo kwenye physical battle yaani ushindani katika utimamu wa mwili. Kama masihara lakini waganda siku zote wanatupiga na wanafanya vizuri Africa kwa sababu wachezaji wao wengi wapo vizuri kiftness. Moja ya adui mkubwa wa soka letu Tanzania kwa vilabu na kwa timu ya Taifa ni ukosefu wa utimamu wa miili iliyoshiba na iliyojengeka kimazoezi kwa wachezji wetu wa kitanzania.
ReplyDeleteTUPAMBANE MPAKA KIELEWEKE.MAFANIKIO YAPO
ReplyDelete