September 14, 2018


Wakati zoezi la kuichangia klabu ya Yanga kupitia michango ya wanachama wake likizidi kushika kasi, Mwanachama anayejulikana kwa jina la Edgar Chibula, amepingana na suala hilo akitaka uchaguzi ufanyike.

Chibula ambaye ni mwanachama wa klabu hiyo, amefunguka na kuwataka viongozi wa Yanga kuhakikisha wanaitisha haraka zoezi la uchaguzi ili kujaza nafasi za viongozi walioachia ngazi nafasi zao.

Kwa mujibu wa Radio One, Mwanachama huyo ameeleza mpaka sasa Yanga imekuwa ikitegemea michango ya wanachama wakati ina uwezo wa kuwa na viongozi ambao wataeleta chachu ya maendeleo ya timu ikishapata viongozi wazuri.

"Klabu kama Yanga haiwezi kutegemea michango ya wanachama pekee, ni klabu kubwa ambayo inatakiwa kufanya uchaguzi ambao utaisaidia Yanga kusimama yenyewe kama ilivyokuwa zamani" alisema.

Mpaka sasa Yanga inakabiliwa na uhaba wa viongozi ambapo wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji wameshajiengua pamoja na Katibu Mkuu pia Mwenyekiti na Makamu.

Wakati huo watani zao wa jadi tayari wameshaanza mchakato huo na kinachosubiriwa hivi sasa ni kurejeshwa kwa fomu za wagombea ambao tayari wameshazichukua tayari kwa kuanza kampeni kabla ya uchahuzi mkuu Novemba 3 2018.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic