September 14, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba umeshangazwa na Shirikisho la Soka Tanzania kuchelewa kuwatumia barua ya kumfungia Meneja wa timu yao, Richard Robert.

Robert alifungiwa na TFF kujihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja sambamba na faini ya kitita cha shilingi za kitanzania, milioni 4.

Baada ya kutangaza adhabu hiyo, taarifa zinasema mpaka sasa TFF hawajatuma barua kwenda Simba inayoeleza kuwa Meneja huyo amefungiwa na kupewa adhabu ya kulipa kiasi hicho cha pesa.

Simba wameshangazwa na kuchelewa kwa barua hiyo kwa maana walitaka kukata rufaa mapema ili kuona namna gani ya kumsaidia Meneja na ikiwezekana kutengua hukumu yake ili aweze kuendelea na kazi kama kawaida.

Meneja huyo alifungiwa na TFF kwa makosa ya kutotii agizo la shirikisho pamoja na kuihujumu Taifa Stars.

1 COMMENTS:

  1. Kwakweli TFF katika suala zima la tangu kufukuzwa kwa wachezaji wa Simba kambini mpaka kumfungia meneja wao inaonesha namna gani viongozi wa taasisi hiyo jinsi gani wanavyofanya kazi kwa mihemko. Kujifanya kutumia sheria na kanuni kuhalalisha maamuzi ya hovyo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic