TFF YAUTAJA UTARATIBU WA KUWAONA MAKAMBO NA KAGERE TAIFA, KUHUSU USALAMA, YOTE KAFUNGUKA
Na George Mganga
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema limeandaa utaratibu mzuri wa kuingia Uwanjani Septemba 30 2018 kushuhudia mechi ya watani wa jadi baina ya Simba na Yanga itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho hilo, Clifford Mario Ndimbo, amesema shirikisho limeandaa utaratibu ambao utamuwezesha kila mtazamaji kuingia kwa utulivu bila kuwepo na bugudha yoyote.
Ndimbo ameeleza kuwa tayari wameshawasiliana na watu wa usalama kwa ajili ya kuhakikisha hali ya amani na utulivu unakuwepo nje na ndani ya uwanja wa taifa kutokana na ukubwa wa mechi hiyo yenye shamrashamra za aina yake.
Ofisa huyo amewataka mashabiki wa mpira kuanza kununua tiketi zao mapema kuanzia Septemba 20 ili kuepuka usumbufu wa kuzitafuta siku ya mchezo jambo ambalo huleta usumbufu.
Timu hizo zinaenda kukutana kwa mara ya kwanza katika msimu huu huku Simba ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo uliopita Aprili 4 2018 ambapo bao hilo liliwekwa kimiani na beki Erasto Nyoni kupitia mpira wa faulo uliopigwa na Shiza Kichuya.
0 COMMENTS:
Post a Comment