September 19, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utawakosa wachezaji watano kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Taifa leo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Dismas Ten amewataja wachezaji Juma Makapu, Ramadhan Kabwili, Pius Buswita na Haji Mwinyi kutokuwepo sababu ya makosa ya kinidhamu.

Ten amesema wachezaji hao waliondolewa na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kwa sababu za kinidhamu ambazo zilimkwaza Mkongo huyo na kuamua kuwapa adhabu ya muda.

Aidha, Yanga itamkosa Juma Mahadhi ambaye bado ni majeruhi ambapo bado anaugulia hali yake mpaka pale atakapoweza kuwa fiti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic