Kauli hiyo ya Ajibu kupelekwa kwenda kucheza soka Ulaya imetolewa na kocha wa mchezaji huyo, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo ambaye anaamini kabisa nyota huyo anajichelewesha tu kuendelea kucheza soka hapa Bongo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera amesema kwamba; “Yeye ni mchezaji ambaye anastahili kabisa kwenda nje kucheza soka na siyo hapa Tanzania kwa sababu ni aina ya wachezaji ambao wanahitajika sana kwani ana kipaji halisi cha soka tofauti na wachezaji wengi.
“Lakini atashindwa kucheza huko kwa sababu moja tu ya kushindwa kujitoa na kutumia nguvu wakati akiwa uwanjani. Ni yeye mwenyewe ambaye anajichelewesha kwenda kucheza nje kwani hastahili kucheza hapa kwa sababu ya jambo hilo la kushindwa kujitoa zaidi nje ya uwezo wake,” alisema Zahera.
Ajibu amefanya mambo makubwa msimu huu baada ya kuhusika kwenye mabao 11 ya timu hiyo na sasa ndiye mchezaji anayetajwa zaidi kuwa ni bora kwenye ligi.
CHANZO: Championi Jumatano
Ibrahim Ajibu alipoondoka Simba kwenda Yanga basi nilijua kesharidhika na maisha ya Bongo. Kweli Yanga wachezaji wanatoka lakini kwa nadra au kwa maneno mengine mpaka mchezaji atumie nguvu kubwa kinganisha na Simba mpaka hao Yanga wenyewe huwafanyia kejeli Simba kwa tabia yao ya kuwaruhusu wachezaji wao muhimu kwenda kujaribu nje wakati mwengine hata kwa mkopo.
ReplyDeleteNonda shaban alikuwa anachezea simba au yanga? Msuva alicheza timu gan? Usiseme hilo kwa kuangalia samatta pekeyake.........
ReplyDeleteSio Ajibu tu pekee yake. Wachezaji wengi wa bongo wanafanya mazoezi ya kawaida sana kama vile wanalazimishwa. Kucheza professional football sio mzaha. Nakumbuka mahojiano ya Samatta na mwandishi mmoja, mara tu aliposajiliwa Tp Mazembe. Alikuwa anasema kwamba, mazoezi yalikuwa magumu na aliona kama yale waliokuwa wakifanya simba yalikuwa chamtoto.
ReplyDelete