KOCHA mkuu wa Simba, Patrick Aussems amelalamikia juu ya ratiba ambayo wanaipitia kikosi chake kwa sasa ya kucheza mechi tatu ndani ya siku nane ambayo haitoi muda wa kupumzika kwa nyota wake.
Simba ndani ya siku nane kuanzia Jumapili iliyopita hadi Jumapili hii watakuwa na kibarua cha kucheza mechi tatu za ligi tofauti. Kikosi hicho kilianza kupambana na Stand United wiki iliyopita kisha leo Jumatano kitacheza tena na Alliance kabla ya kumaliza Jumapili hii kucheza tena na Ruvu Shooting.
Kocha huyo ameliambia Championi Jumatano, kuwa ratiba hiyo kwao haijakaa sawa kwani inaweza kusababisha majeraha kwa wachezaji wake kwa sababu haitoi muda kabisa wa wao kupumzika baada ya kumaliza mechi moja.
“Kwa sasa tuna ratiba ngumu kidogo kwani ni ndani ya muda mfupi tu tunacheza kisha tutacheza tena. Utaona tumecheza Jumapili iliyopita lakini baada ya siku chache tu tunacheza tena na baada ya hapo tutahitajika tucheze tena.
“Kitu hicho ni kigumu kidogo kwani kinaweza kusababisha matatizo kwa wachezaji kwa sababu hakutakuwa na ratiba ya kupumzika wanapomaliza mechi moja kwenda nyingine,” alisema Mbelgiji huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Asipuuzwe kwani nnaimani kuwa anauujuzi zaidi juu hao waliokuwepo TFF. Wachezaji wa ligi ndio wachezaji wa timu ya Taifa lazima busara itumike tusiyachukulie mazingira ya Uingereza ndio ya tanzania.
ReplyDeleteKwan anacheza simba peke yake mbona team zote ivyo ivyo......halaf simba c wana kikosi kipana wakomae tu hp bongo c ulaya
DeleteTatizo mashabiki wengi wa Simba ni kauli ya Rage,nimeisahau vile sijuhi inasemaje?
ReplyDelete