October 29, 2018



Ofisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameibuka na kuwaponda kiaina Simba kwa kusema kuwa ushindi wa mabao 5-0 walioupata haimaanishi wana uwezo mkubwa.


Ruvu Shooting waliwakaribisha Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Simba walifanikiwa kuchukua pointi tatu, Bwire amesema bado ana amini timu yake ina uwezo wa kufanya vizuri.

"Ushindi wakati mwingine siyo uwezo ni mpango wa Mungu, kumbukeni askari wenye kila sifa ya uaskari, askari wale wa Sham waliotumwa kwenda kumkamata Elia katika Taifa la Israel walishindwa kumkamata siyo kwamba hawakuwa na uwezo bali ulikuwa ni mpango wa Mungu, Subirini kuche, tutaelewana tu," alisema.

Kabla ya mchezo Bwire alijipambanua kuwa timu yake itafanikiwa kuwashangaza mashabiki wa Simba kwa kuwapapasasquare kama kauli mbio yao inavyosema hali iliyofanya uongozi wa Simba kukaa kimya na kusubiri dakika 90 ziamue.

10 COMMENTS:

  1. Hana lolote huyo Masau Bwire, sio mtu wa michezo. Kwa mtu yeyote unayejua mchezo wa mpira, lazima utaona kabisa pengo lilopo kati ya Simba na Ruvu shooting ni kubwa. Kiwango cha Simba sio cha Ruvu. Bado sana Ruvu kulinganishwa na Simba. Mwaka jana 7-0 leo 5-0 utasemaje hapo sasa? Kama angekuwa ni fundi wa mpira angesema ukweli kwamba hawajafikia level ya Simaba

    ReplyDelete
  2. Masau Bwire Mzee Wa Maneno Mengi Uwezo Wa Timu Yako Ni Mdogo Sana Kifedha Kiuchezaji Na Hata Wachezaji Wenyewe Bado Viwango Vyao Ni Vidogo Sana Kulinganisha Na Simba "Simba Nguvu Moja" {Simba Njaa Haizoeleki}

    ReplyDelete
  3. Vitendo vinamtosha muacheni bhana,endapo ligi itaendelea na mwendo huu kwa timu hizi tatu kushinda mpaka mwisho Wa ligi itakuaje?

    ReplyDelete
  4. Vitendo vinamtosha muacheni bhana,endapo ligi itaendelea na mwendo huu kwa timu hizi tatu kushinda mpaka mwisho Wa ligi itakuaje?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haitawezekana...Yanga wakitoka tu nje ya Dar hawatashinda..kuchezea uwanja wa nyumbani inasaidia Ingekuwa Chamazi Jana mbona Singida angefungwa zaidi ya moja...rafiki usitegemee Yanga itaendelea shinda...Na mechi ya pili ya Simba akipaki basu kama alivyofanya...atapigwa hamsa

      Delete
  5. Yaani jana nilipenda Ruvu shooting wapigwe kumi hivi😅😅😅😅

    ReplyDelete
  6. Ndio timu inayofungwa goli nyingi na Simba.Mwaka jana 10 na mwaka huu zikipungu sana 7

    ReplyDelete
  7. Nakubaliana wakati mwingine ushindi ni mpango wa Mungu hususani kwa timu Yanga...mechi nyingi wanazidiwa umiliki wa mpira lakini wanaendelea kushinda tu! Ila kwa Jana siyo mpango wa Mungu!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic