Mshambuliaji wa Azam FC, Donald Ngoma aliyesajiliwa akitokea Yanga, ameanza kurejea katika ubora wake baada ya kusumbuliwa na majeraha ya goti kwa muda mrefu, amekuwa msaada ndani ya timu kwa kufunga na kuweza kutoa pasi ya bao.
Mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania, Ngoma alitengeneza pasi ya mwisho ya bao la ushindi ambalo lilifungwa naYahya Zayd, amefikisha bao la pili, bao lake la kwanza aifunga dhidi ya Coastal Union, la pili aliwafunga Singida United nyumbani katika Uwanja wa Namfua.
Kocha Mkuu wa Azam, Hans Pluijm amesema amempa Ngoma kazi mbili uwanjani akishindwa kufanya moja ni lazima afanye ya pili ili kuisaidia timu kupata matokeo.
"Ngoma ni mchezaji mzuri, nimemwambia akiwa uwanjani kama atashindwa kufunga basi anatakiwa atoe pasi ambayo ataleta bao la ushindi hicho ndicho anachokifanya," alisema.
Azam wameanza msimu huu ni vizuri kwa kuwa katika michezo 11 waliyocheza hawajapoteza, wametoa sare tatu, wamejikusanyia jumla ya pointi 27 na kuwa vinara wa ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment