October 23, 2018


Nahodha wa Simba, John Bocco yupo fiti kuwavaa wapinzani wa timu ya Alliance, baada ya kukamilisha adhabu ya kadi nyekundu aliyopata katika mchezo dhidi ya Mwadui.

Bocco alikosa mechi tatu kwa ambazo Simba walicheza ikiwa ni pamoja na Yanga, African Lyon Stand United, Simba walifanikiwa kushinda michezo miwili na kutoa sare dhidi ya Yanga.

Kocha Mkuu Patrick Aussems amesema kurejea kwa Bocco kunazidi kuongeza nguvu ya ushindani kwa kuwa ni mchezaji mwenye uwezo wa kubadilisha matokeo na kuongoza akiwa uwanjani.

"Ni mchezaji mzuri ambaye ana kipaji akiwa ndani ya uwanja na nje kwa kuwaongoza wachezaji wenzake hivyo kurejea kwake kunaongeza nguvu ndani ya kikosi katika kutafuta ushindi" alisema.

Simba wamecheza michezo nane wameshinda mitano, wametoa sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja, kesho watakuwa uwanja wa taifa wakicheza na Alliance.

6 COMMENTS:

  1. Yeah Alliance wajiandae kiakili,chakuwashauri waondoe mchecheto wanao uwezo wakuonyesha Maajabu siku ya kesho nina imani watashinda endapo watazingatia waliyofundishwa na kocha,kiukweli simba ni timu ya kawaida sana tatizo ni hofu kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeongea kishabiki, lakini moto unaujua

      Delete
  2. Yeah Alliance wajiandae kiakili,chakuwashauri waondoe mchecheto wanao uwezo wakuonyesha Maajabu siku ya kesho nina imani watashinda endapo watazingatia waliyofundishwa na kocha,kiukweli simba ni timu ya kawaida sana tatizo ni hofu kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba timu ya kawaida eeee? Wadanganye Alliance tu.

      Delete
  3. timu ya kawaida iliyowafanya mpaki treni, mtavionea hivyo vitimu vidogo kwani hata nyota wenu wanawika kwenye timu hizo tu

    ReplyDelete
  4. Hakika, wanawafungukia timu ndogo tu, kwa simba wachezaji wote walikuwa ni makipa siku ile. pamoja na kupaki bado mchezaji akaonekana Kakolanya peke yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic