October 4, 2018


Mshambuliaji wa Monaco na Colombia Radamel Falcao, 32, amehusishwa na kuhama kwenda klabu ya David Beckham ya Inter Miami wakati timu hiyo itajiunga na MLS mwaka 2020. (Sport)

Gareth Southgate atasaini mkataba ndani ya saa 24 zinazokuja kusalia kama meneja wa England hadi mwaka 2022. (Mirror)

Mkataba huo ambao unaripotiwa kuwa wa thamani ya paunia milioni 3 kwa mwaka, utamweka kwenye klabu meneja huyo mwenye miaka 48 hadi baada ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Wamiliki wa Manchester United, familia ya Glazer bado wanamuunga mkono Jose Mourinho kama meneja wa klabu licha ya nafasi hiyo kutiliwa shaka kufuatia matokeo mabaya ya United ya kuanza kwa msimu. (ESPN)

Manchester City wamefanya mikutano kadhaa na polisi huko Merseyside na huenda wakaweka siri njia ambayo watatumika siku ya Jumamosi na Liverpool huko Anfield kuzuia kurudia kile kilichotokea mismu uliopita wakati wa robo fainali ya Ligi ya mabingwa. (Sun)

Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23, amekataa ofa ya tatu ya thamani ya pauni milioni 6.38 kuongeza mkataba wake kwenye klabu hiyo. (Bein Sport)

Meneja wa Shakhtar Donetsk, Paulo Fonseca ni mmoja wa wale wanaweza kuchukua nafasi huko Aston Villa baada ya Steve Bruce kufutwa siku ya Jumatano. (Birmingham Mail)


Mchezaji wa zamani wa Arsenal na naibu meneja wa Ubelgiji Thierry Henry pia naye anataka kazi huko Aston Villa. (Mirror)

Mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour angeinunua Newcastle United badala ya Man City miaka 10 iliyopita. (Manchester Evening News)
Kiungo wa kati wa Real Madrid Isco, 26, anasema anakaribia kupona kabisa baada ya kufanyiwa upasuaji. (AS)
Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll anatarajiwa kutejae baada ya kupata jeraha. Hajaichezea Hammers tangu mwezi Mei. (Mirror)
Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic