KIUNGO ARSENAL KUIKOSA EUROPA LEAGUE
Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan hataweza kuwachezea katika mechi yaligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, dhidi ya klabu ya Qarabag.
Hii ni kutokana na uhasama wa kisiasa ambao umekuwa ukiendelea kati ya taifa lake la Armenia na Azerbaijan.
kwa mujibu wa BBC, Mkhitaryan, 29, hakuweza kusafiri pamoja na wachezaji wenzake kwenda mji mkuu wa taifa hilo, Baku, Jumatano kwa ajili ya mechi hiyo ya Alhamisi.
Hakuna uhusiano wowote wa kidiplomasia kati ya Armenia na Azerbaijan kutokana na mzozo wa muda mrefu kuhusu eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh.
"Hawezi kusafiri huko," meneja wa Arsenal Unai Emery alikiri hilo.
"Tuko hapa, wachezaji wana mtazamo mwema na wamejiandaa vyema kucheza."
Gunners watakutana na Qarabag katika mechi ya Kundi E saa mbili kasoro dakika tano saa za Afrika Mashariki.
Uefa wameambia BBC kwamba uamuzi wa pamoja ulifanywa na Arsenal na Mkhitaryan kwamba asisafiri kwa sababu za kiusalama.
0 COMMENTS:
Post a Comment