October 23, 2018







Mshambuliaji Obrey Chirwa tayari yuko jijini Dar es Salaam na inaelezwa chanzo ni kutolipwa baadhi ya fedha zake za usajili na kucheleweshewa mshahara kwa takribani miezi mitatu akiwa na klabu ya Nogoom El Mostakbal nchini Misri.

Kutokana na hatua hiyo, Chirwa raia wa Zambia, ameamua kuvunja mkataba baada ya kukaa kwa miezi mitatu na kuona mambo yanazidi kuwa magumu.

Imeelezwa, klabu hiyo ya Ogoom El Mostakbal ndiyo ilimfanya Chirwa kuondoka Yanga.

"Chirwa amerejea sababu mkataba umevunjika," kilieleza chanzo. Unajua jamaa wamemsumbua kumlipa fedha za usajili na wakati mwingine mshahara, ndiyo maana ameamua kureea nchini na hata kama akiamua kuondoka, atarudi kwao Zambia lakini si Misri."

Pamoja na hivyo, tokea ametua ogoom El Mostakbal mambo yake hayakuwa mazuri hasa katika suala la malipo.


Kutokana na hali hiyo, Chirwa aliamua kurejea Tanzania kumtembelea Donald Ngoma, rafiki yake walioyecheza pamoja Azam FC.

Chirwa alikuwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa Yanga kabla ya kuamua kuondoka kwenda Misri.

10 COMMENTS:

  1. Daah! Chirwa na Ngoma walipata kucheza pamoja Azam!!? Hiyo ilikuwa mwaka gani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. msipende kukuza mambo....alitaka kumaanisha Platnum

      Delete
  2. hata mm nashangaa labda wakitukumbusha vzr

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakutaka kuma an kumaanisha hivyo nyie hamjawahi kukosea kutype???? Izo ni human error za kawaida tu ata wewe unakoseaga sanaa tuu

      Delete
    2. Hakutaka kumaanisha hivyo nyie hamjawahi kukosea kutype???? Izo ni human error za kawaida tu ata wewe unakoseaga sanaa tuu

      Delete
    3. Typing error haiko hivyo. Typing error ni kama vile ulidhamilia kuandika neno "kote badala yake ukaandika "teko". Kusema Chirwa na Ngoma walicheza wote Azam hiyo sio typing error ni umbumbumbu wa kutokujua mambo. Manake kuandika sio kama vile kutamka neno. Kuandika, unafirikilia unachokiandika, kisha unarudia kukisoma kabla hujaamua kukichapicha. Acheni mambo ya kukurupuka lazima usome tena habari yako na kuonekana hujui unachokiandika.

      Delete
  3. Timu itayomrudixha hpa bongo chirwa itapata taabu maana jamaa mkichelewa kumlipa tu mxhahara in xhida hana uvumilivu hata km timu inamlipa matumizi yy ni mgomo tu hata mazoezi

    ReplyDelete
  4. Ni ujinga mtupu na huyo Chirwa pumbavu kubwa. Aliondoka hapa bongo kwa mbwembwe nyingi eti anakwenda Ismailia? Hovyoo, Na wa kandambili wakileta kejeli kwa Simba haina uwezo wa kumajili? Na Simba kwa kuonesha jeuri wakamleta mzambia bora zaidi na gharama kuliko Chirwa. Ujinga wake kama kweli Msimbazi walimuhitaji angekuwa keshasahau machungu ya kulilia mshahara wake kila mwezi.

    ReplyDelete
  5. Chirwa alikuwa analipwa dola 3500 wakati akiwa Yanga na alisajiliwa kwa dola 100,000.Sasa utamlinganishaje na Chama aliyesajiliwa kwa dola 50,000 na analipwa mshahara wa dola 2500?
    Nyie watu wa Simba pambaneni na hali yenu uwanjani maana yajayo yanamaudhi kwa msimbazi!

    ReplyDelete
  6. MNASHANGAA HUYU MWANDISHI KWANI NI MJINGA HASA, HABARI ZAKE SIKU ZOTE NI UPUUZI TU

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic