October 23, 2018



Mlinda mlango wa timu ya KMC, Juma Kaseja amesema hana mashaka  na wachezaji wa timu za Tanzania kwa kuwa ana uzoefu wa muda mrefu ndani ya ligi.


Kaseja amesema washambuliaji wa ndani na nje wote uwezo wao ni sawa tayari ameshacheza mechi nyingi za kitaifa na kimataifa bado ana nafasi ya kuweza kuisadia timu yake dhidi ya timu zote ligi kuu ikiwa ni pamoja na Simba na Yanga.

"Bado sijaona mshambuliaji mwenye uwezo wa kunitisha ndani na nje ya ligi,uzoefu wangu unatosha kunifanya nizidi kuwa imara,nitapambana kwa ajili ya timu ili kuweza kuleta ushindani ndani ya ligi," alisema.

Kwa sasa, Kaseja ni mmoja wa wachezaji wakongwe zaidi katika Ligi Kuu Bara.

Akiwa katika ligi hiyo kwa zaidi ya miaka 15, Kaseja amezichezea timu za Moro United, Simba, Kagera Sugar na sasa KMC ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic