October 17, 2018



Mashabiki wa soka nchini England wamecharuka dhidi ya beki Sergio Ramos wa Hispania kwamba amezidi mambo ya kihuni.

Mashabiki hao wamemshambulia Ramos mitandaoni wakimtuhumu kumkanyaga Rahim Sterling katika mechi ambayo Hispania ilipoteza kwa mabao 3-2.

Sterling anayekipiga Manchester City alifunga mabao mawili katika mechi hiyo na Ramos alimkanyaga akiwa amekaa chini.

Picha za video Ramos anayecheza Real Madrid akimkanyaga Sterling ingawa yeye anataka kuonyesha kuwa ilikuwa bahati mbaya.

Mashabiki hao wanapata jazba kwa kuwa jambo hilo linawakumbusha rafu mbaya aliyocheza Ramos dhidi ya Mohamed Salah katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Katika mechi hiyo Salah alilazimika kwenda benchi na inaonekana ukawa msaada kwa Madrid kuitwanga Liverpool iliyokuwa ikionekana ingefanya maajabu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic