October 3, 2018


Na George Mganga

Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga nchini, Bakili Makele ameibuka na kutoa pongezi kwa wapenzi, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa ligi dhidi ya Simba.

Makele amefurahishwa na ujio wa mashabiki hao kwa namna walivyojitokeza na kutoa hamasa wa timu yao licha ya kupitiwa na wakati wa mpito.

Mwenyekiti Makele ametoa pongezi hizo akiamini ujio huo wa wingi utazidi kuonekana pia kwenye mechi zingine ukiachana na Simba jambo ambalo litasaidia klabu kupata mapato haswa kwa mechi zake za nyumbani.

Aidha, Makele ametoa pongezi kwa wachezaji wake namna walivyojituma katika mchezo huo licha ya kuzidiwa na Simba kwa kusema walipambana.

Yanga hivi sasa inajiandaa na mchezo ujao dhidi ya Mbao FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki kusaka pointi tatu ili kuendelea kupigania harakati za ubingwa wa ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic