October 29, 2018


Mchezaji Emmanuel Okwi alifunga 'Hat-trick' na kuwa mchezaji wa pili kufunga msimu huu, Alex Kitenge wa Stand United alifanya hivyo kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga, maajabu ya mabao matatu ya Okwi yanaingia mpaka kwenye takwimu kwa kuwa katika kila sehemu kuna namba tatu.

Kwenye mashuti yaliyokwenda nje ukiangalia huwezi kupata namba tatu ila ukitoa idadi ya Simba ya mashuti ambayo ni 8 na ile ya Ruvu Shooting 5 utapata jibu, kwa upande wa kadi za njano ukijumlisha kadi zote utapata jibu ambalo ni tatu sawa na mabao ya Okwi, takwimu zipo kama ifuatavyo :-

Mashuti yaliyolenga lango:- Ruvu Shooting 3-9 Simba.

Mashuti nje ya lango:- Ruvu Shooting 5-8 Simba.

Kona:- Ruvu Shooting  3-3 Simba .

Kuotea:- Ruvu Shooting 3-6 Simba .

Kadi ya njano:- Ruvu Shooting 2-1 Simba.

Faulo:- Ruvu Shooting 16-13 Simba.

Umiliki wa Mpira:- Ruvu Shooting 37%-63% Simba.

Ushindi wa mabao 5-0 umewafanya Simba waweze kufikisha pointi 23 baada ya kucheza michezo 10 kwenye Ligi Kuu Bara, wanashika nafasi ya pili huku vinara ni Azam FC wana pointi 27.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic