October 10, 2018


Mtayarishaji wa muziki Maarufu, wa B’ Hitz Record, Pancho Latino, maarufu kama Mafia, amefariki dunia jana jioni kwenye ajali ya kuzama na maji wakati akiogelea kwenye kisiwa cha Mbudya  jiijini Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu  umehifadhiwa katika hospitali ya Lugalo kwa uchunguzi zaidi.

Hali ya majonzi ni kubwa kutoka kwa marafiki aliokuwa nao Mbudya, ndugu jamaa na marafiki. 

Mmiliki wa Studio ya B’ Hitz Hammy B ni mmoja ya watu walioonekana katika hospitali ya Lugalo muda huu.

Latino atakumbukwa kwa kazi zake kibao alizowahi kuzifanya kama vile Nangoja Ageuke ya AY na FA, Bado Nipo Nipo ya FA, Dar es Salaam Stand Up ya Chid Benz, Baadaye Sana ya Mabeste, Amore ya Baby Madaha, Show za Joh ya Joh Makini, Msiache Kuongea ya FA pamoja na Closer ya Vee Money.

Taarifa zaidi zinakuja. Mungu ailaze roho ya mpendwa wetu mahala pema peponi Amen.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic