October 18, 2018


Nyota wa Brazil Neymar, 26, anajutia uamuzi wake wa kuondoka Barcelona na kujiunga na Paris St-Germain na kwamba yuko radhi kurejea Nou Camp mwisho wa msimu huu. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania).

Wachezaji mahiri wa Ufaransa katika klabu ya Barcelona wanamtaka kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, kujiunga na klabu hiyo. (Mail).

Manchester United na Liverpool wanamfuatilia winga wa PSV Steven Bergwijn wa miaka 21. (De Telegraaf, via Sun).

Arsenal ni klabu ya hivi punde kuhusishwa na uhamisho wa kiungo wa kati wa kimataifa wa Italia na Cagliari, Nicolo Barella, 21. (Gazetta dello Sport, via Football London).

Vilabu vya Juventus, Barcelona na Manchester City vinapania kumnunua mlinzi wa Ajax Matthijs De Ligt,19, ambaye huenda akagharimu karibu euro milioni 50. (Goal.com).

Agenti wa mlinzi wa Juventu, Daniele Rugani, anadai kuwa mchezaji huyo wa kimatafa wa Italia mwenye umri wa miaka 24 alikataa kuhamia Chelsea msimu uliopita wa joto. (Calciomercato).

Tetesi za kuhusishwa kwa mlinzi wa kimataifa wa Slovakia na Inter Milan, Milan Skriniar, 23, na vilabu vya Manchester United na Manchester City, zinaashiria kiungo huyo huenda akajiunga na ligi ya Primia. (La Gazetta, via Calciomercato)


Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic