RONALDO MATATANI KWA TUHUMA ZA KUBAKA
Mwanamke mmoja, Kathryn Mayorga, amejitokeza na kusema mwanasoka, raia wa Ureno, Cristiano Ronaldo alimbaka mwaka 2009 katika hoteli moja jijini Las Vegas, Marekani.
Baada ya tukio hilo mwanamke huyo akiri kupewa Dola za Marekani, $375,000 kama malipo ya kutakiwa kukaa kimya na kutozungumzia suala hilo.
Hata hivyo, Ronaldo, kupitia video ya moja kwa moja katika mtandao wa Instagram, alikana tuhuma madai hayo akisema ni ya uongo na yametengenezwa na watu wanaotafuta umaarufu.
Katika hati ya madai iliyofunguliwa Ijumaa iliyopita katika Wilaya ya Clark, inadaiwa Ronald aliomba msamaha “akisema alikuwa amesikitishwa na kitendo hicho na kwamba yeye alikuwa mstarabu.”
Vilevile inadai kwamba mwanasoka huyo alikiri mbele ya mawakili wake kwamba ni kweli mwanamke huyo alikuwa akisema hataki na alikuwa anamwambia aache mara moja ukatili huo.
Hati ya mashitaka inasema Mayorga alikutana na Ronaldo katika hoteli iitwayo Palms Hotel and Casino, Juni 13, 2009, ambapo Ronaldo alimkaribisha mwanamke huyo na marafiki zake wa kike kwenye sehemu aliyofikia na mwanasoka huyo akamwomba aungane na kundi la wenzake katika jacuzzi kwa ajili ya burudani ya kuoga ambapo alimpa bukta na T-shirt.
Mwanamke huyo alipokwenda katika chumba cha kubadilishia nguo, Ronald alimwendea na kumwomba wafanye ngono ya mdomo, alipokataa, alimvutia ndani ya chumba chake cha kulala na kumbaka huku akipiga makelele ya “Hapana, hapana, hapana.”
Siku hiyohiyo, aliripoti tukio hilo polisi na kwenda kupimwa hospsitali kuhusu tukio hilo.
Kesi inaendelea kuunguruma.
0 COMMENTS:
Post a Comment