October 1, 2018


Na Haji Manara

Mpira ni mchezo wa hadharani hauchezewi chumbani, sijaelewa Kocha aliposema walikuja kulinda huku akiruhusu Simba watengeneze nafasi.

Kwa kadri nnavyofahamu unapocheza mpira wa kujilinda, hupaswi kuruhusu mpinzani wako kutengeneza nafasi na humpi hyo nafasi.

Kocha anajisifu wakati umepigiwa mipira iliyolenga lango na ambayo haijalenga 10 kumi, fikiria zingeingia! 

Kocha anaekuja na mipango ya kujihami hakupi nafasi ya kulisogea goli, utaishia nje ya 18 hii ni hadaa kubwa.

Hivi angewaeleza nini kama zile tageti zingejaa? Kwangu mimi narudia nyota wa mchezo ni Kakolanya na bahati tu si kwa mbinu zile za kuruhusu shots on & off 20.

21 COMMENTS:

  1. Manara naungana na wewe kwa 100% kwa kweli Kakolanya sivyo walivyombeza siku za nyuma jana amefanyakazi kubwa sana kama kipa bora. Na kama asingekuwa makini leo nafikiri timuatimua ya Yanga ingekuwa kubwa kuliko kama inavyoelezwa wakati huu.

    Protas
    Iringa-Tanzania

    ReplyDelete
  2. manara waachie makocha kazi yao wewe endeleza propaganda tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo kocha ni fala anazidiwa na sahabiki wa kawaida ktk kutoa tathmni ya mchezo

      Delete
  3. Bongo ni mipasho tu na sio mpira wala ufundi,Jose Mourinho alikuwa ana park bus lakini anapigiwa shots on targets hata 20 na akihojiwa anasema niliingia na mbinu ya kukaba na kuwaacha wacheze mpira,let them proffesionals be proffesionals in their career and let remain with ours.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hakuna proffessional ya hivyo brotherm sema huyo kocha wa yanga na mourinho walishindwa la kusema na kuamua kuongea hayo

      Delete
  4. mpira umeisha wote tumeona kocha yupo sawa mfumo uliotumika ni kulinda so manara unataka kutuambia hujaona pia kumbuka kakolaya alidajiliwa kufanya aliokua akifanya.

    ReplyDelete
  5. Mtasema sana huyo ndo profosheno zahera kocha msaidizi wa kongo mtatoka sana povu mwaka huu.

    ReplyDelete
  6. Hivi watu wanashangaa jana mbona mechi ya Arsenal vs Manchester United. Short ontagert ilikuwa 16 kwa 4 ball possession 77 Kwak 23 lakini matokeo 1 - 3 kila timu ina mbinu zake namuomba Manara aweke statistics za mechi ya Zamaleikh na Simba kule Cairo ndio tutamuona mkweli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nadhani unaposema ulienda kuiachia timu icheze moira na wewe kulinda unatakiwa uimarishe uwezo wa kupokonya mpira na kufanya counter attack na si vinginevyo. Yanga jana wamefanya shambulizi gani la maana?

      Delete
  7. Chizi huyo jamani na aliyemloga kafa....lengo lilikuwa kutoruhusu gol. Hakukuwa na lengo la kuzia on & off taget yako...na kweli lengo likatimia hawakuruhusu goli

    ReplyDelete
  8. Ninachokusifu Manara umebobea kwenye mipasho. Una mipasho mpaka umepitiliza , Mchezo mliocheza jana ndio mliocheza na Ndanda mkayoa drootasa na ndio Mliocheza na Mbao mkafungwa moja bila.

    ReplyDelete
  9. Baada ya Mzee Yussuf kujiuzulu taarab nadhani msemaji maarufu anajiandaa kuichukua hiyo nafasi. Ukimkuta mfagiaji hospitali anajadili cheti kilichoandikwa na daktari kwa mgonjwa usijiulize maswali mengi bali tambua anaemsikiliza pasi ubishi atakuwa mgonjwa zaidi.
    Tuwaachie wataalamu waseme vinginevyo tutabakia na ngeli nyingi

    ReplyDelete
  10. Msemaji vs kocha, msemaji Wa Simba vs kocha Wa Yanga.
    Tafsiri, anaomba aongelee mambo ya yanga huku mambo ya Simba yakimshinda.

    ReplyDelete
  11. Msemaji vs kocha, msemaji Wa Simba vs kocha Wa Yanga.
    Tafsiri, anaomba aongelee mambo ya yanga huku mambo ya Simba yakimshinda.

    ReplyDelete
  12. Hayo ni maneno ya mkosaji.Sheikh wangu huyu asiongelee kabisa hizo shot on target zisizozaa matunda wala asimlaumu kocha wa Yanga,alaumu na kushangaa uzembe wa washambuliaji wake.

    ReplyDelete
  13. Baada ya kushangaa kocha wako mechi 6 point 11 unamshangaa kocha wa YANGA mechi 5 point 13 wewe kweli juha

    ReplyDelete
  14. huyu manara bwege sana.......sasa hizo shorts on target zake zimemsaidia nini?

    ReplyDelete
  15. He!manara kumbe ximba wakipiga xhoot juu kabixa ya goli LA yanga unawaona wako vzri,mlikaribixhwa mxhambulie kixha mfungwe goli LA kuxhitukiza kma LA ubao LA mipango ya yanga pale mbele iligoma kutoka na kutumia mxhambuliaji mmoja ambae alikoxa kiungo was kumlixha mipira bahati yko hilo hujalijua mpk sasa unaleta taraabu tu

    ReplyDelete
  16. Kwanza cha kujiuliza kwanini Yanga iende uwanjani kwa lengo la kujilinda? Kwani haya ni mashindano ya mtoano ya ugenini na Nyumbami? Ligi bado mbichi kwanini kocha awe na mawazo ya kuiogopa Simba kiasi hicho? Hayo maneno ya kujigamba kuwa Simba ni timu ya kawaida basi ni unafiki mkubwa. Yanga wataendelea kuchonga lakini kwa Simba hii watapigwa bao nje na ndani ya uwanja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic