October 2, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba umelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuangalia upya suala la mapato ya mechi za ligi kwenda kwa mwenyeji pekee.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema suala hilo bado linapaswa kufanyiwa mapitio mapya kulingana na hali ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu.

Manara ameeleza kuwa ni vema TFF ikajaribu kupitia upya kuona faida na hasara zake kwani wanaweza kuja na mawazo mengine ambayo yatakuwa yanalenga kuzipa faida timu zote.

TFF ilitangaza mabadiliko ya mapato yanayotokana na viingilio vya mashabiki uwanjani kwa msimu huu yote kwenda kwa mwenyeji pekee badala ya mgawanyo kwa timu husika.

"nadhani TFF wanapaswa kuliangalia vema hili suala kwa kulipitia upya ili kuona faida na hasara zake, pengine wanaweza kuja na mtazamo mpya. Ngoja tuone kwa msimu huu pengine wanaweza wakajifunza kitu" alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic