NA SALEH ALLY
KUNA nani anataka amlaumu nani kuhusiana na Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Cape Verde katika mechi ya kuwania kufuzu kucheza Afcon mwakani?
Anayetaka kumlaumu mmoja, wawili au wote yeye amelifanyia nini taifa hili? Kama amelifanyia kitu anapaswa kulaumu au kuwasaidia waliokosea ili wafuate kizuri ambacho aliwahi kufanya?
Taifa Stars imecheza vibaya mchezo wake dhidi ya Cape Verde, imecheza kwa kiwango cha chini kabisa ukianza na mabeki, viungo na hata washambuliaji. Hilo halina ubishi na sote tuliona hasa wale ambao walitaka kuyaona mambo kwa umbali zaidi.
Unapoangalia mpira unaweza kuchagua kuangalia kile ambacho kinakuvutia na unataka uangalie vipi. Wako wanaangalia wakitaka kufurahi lakini wanachagua kujifunza na wa aina hii huangalia ndani zaidi kwa kila kinachotokea.
Wale ambao wanapenda kulaumu hutaka kuona timu inashinda, hawataki kuona wachezaji wao wanakosea, wanashindwa au wameteleza. Mara nyingi hata timu ikishinda bado watakuwa na vitu kadhaa angalau vya kulaumu.
Watu hawa ndiyo wale wapo kwa ajili ya kulaumu tu. Kazi yao ni kuchambua ubaya wa kila kilichotokea bila ya kuangalia kulikuwa na uzuri angalau kidogo. Kama haukuwepo, lawama zao huwa zisizo na msaada kwa kuwa hawashauri hata kipi kingetokea.
Kumlaumu kocha, kuwalaumu wachezaji na kadhalika umekuwa ugonjwa wetu na huenda anayelaumu sana huonekana ni mtu mzuri sana. Huonekana ni mtu mwenye uchungu sana.
Wakati mwingine vizuri kufikisha ujumbe bila ya lawama, maana unayemlaumu unaweza kumchanganya zaidi na hata kile unachomshauri kisimfikie vizuri na kikimfikia asikipokee vizuri.
Swali langu moja kwenu nyote mnaolaumu kupindukia kutokana na Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Cape Verde. Kwamba je, mnaamini kuna mchezaji wa Taifa Stars anaweza akawa anataka kufungwa au kutocheza vizuri kwa makusudi?
Ukisema ndiyo, utakuwa unachekesha sana. Tunajua wanataka kushinda lakini siku hazifanani, Kocha Emmanuel Amunike amekiri, walicheza katika kiwango cha chini kabisa.
Sayansi ya mpira inategemeana, mabeki kuruhusu mabao mawili mapema, walichangia kuwachanganya pia washambulizi maana wakawa na presha kubwa. Utaona nahodha Mbwana Samatta alipambana angalau kupata bao moja. Viungo hawakuwa vizuri mawasiliano yakapotea na kuwapoteza washambulizi.
Mwisho uliona ushirikiano wa mbele ulivurugika na mambo hayakuwa sawa. Kocha amekubali, hawakuwa vizuri. Kama yote haya tumeyaona, Stars ambayo inajiandaa na mechi dhidi ya Cape Verde kesho Jumanne inapaswa kulaumiwa au kupewa ushauri na kuungwa mkono?
Ukiendelea kulaumu tu faida yake ni ipi? Una timu nyingine ya taifa inayokufurahisha zaidi na si Taifa Stars? Basi nenda.
Watakaobaki, basi tuamini timu yetu ya taifa haijawahi kufungwa kila mechi. Kuna mechi huwa inashinda na kutufurahisha, vipi leo kulaumu tu utafikiri kuna timu haikuwahi kufungwa? Ndiyo maana nasema kama kuna jambo la kushirikiana timu icheze kwa morali Jumanne, lifanyike sasa.
Kuendelea kuwashambulia wachezaji, wao watakuwa waliharibu Cape Verde na sisi mashabiki tuharibu Dar es Salaam mapema. Kama watapoteza hapa nyumbani, sisi ndiyo tutakuwa chanzo.
Tayari tuko katikati ya mapambano. Inawezekana kama kuna jambo tunataka kunyumbulisha, basi baada ya Jumanne. Lakini sasa tuwaamini wachezaji wetu na kuwapa nafasi, kuwaunga mkono na kuwasisitiza, tuko nao katika vita hii.
Wameianza na kuteleza huko Cape Verde. Sasa ni zamu ya kulipa kisasi na kujitegenezea matumaini upya ya kucheza Afcon.
Nafasi bado ipo kama Stars italipa kisasi kwa kuifunga Cape Verde. Halafu ina mechi nyingine mbili, moja ugenini na Lesotho na moja nyumbani na Uganda. Kumbuka Taifa Stars ikifeli, kama ni Mtanzania, umo. Ikifanikiwa basi nawe hata kama huchezi utajivunia. Hivyo waunge wanaopigana kwa ajili ya taifa lako.
No comment, lets unit to overcome our opponent!
ReplyDeleteNi kweli lakini kocha awatumie wachezaji wenye uzoefu zaidi kama nyoni, coton, chilunda,wanaweza kuongeza kitu
ReplyDeleteTatizo sio kulaumu au kutolaumu. Taifa Stars ni ya 140 kwenye viwango bus FIFA,Cape Verde ni ya 67.Hawakufika hapo kwa kelele na majivuno bali juhudi,uvumilivu na mipango mizuri ya kuendeleza mpira nchini kwao tena wakiwa hawana hata ligi ya ndani. Sisi tumekalia maneno nä kujisifu .Tukubali udhaifu wetu. Tujipange na ikiwa tupo tayari kufanikiwa tuwe tayari pia kutofanikiwa.Tuache kushinda kwenye magazeti kama Uingereza matumaini kibao bila uhalisia. Kama tunastahili kuwepo kwenye fainali za nchi wanachama wa CAF tutashinda michezo yetu 2 na kusubiri hatma yetu .Vinginevyo tujipange upya.Hakuna shortcut kwenye mafanikio.
ReplyDeleteSaleh nawe umekuwa mwanasiasa tena siasa zilizopitwa na wakati sio za wakati huu wa Magufuli. Katika siasa watanzania kwa kipindi kirefu tuliaminishwa nchi yetu ni masikini na hatukuwa na uwezo wa kujiendeleza na akili zetu zikiganda kufikiria na kungojea misaada kutoka nje na kwa kiasi fulani watanzania katika kujipa moyo kwenye hali ya kukata tamaa na maisha kila kitu husukumiwa Mungu kuwa ndio aliejaalia kuwa na hali duni na kubakia kuridhika na maisha ya mchangani kitu ambacho ni zambi kwani Mungu kwa jinsi alivyomuumba binaadamu bila ya kuwa na chochote basi ni utajiri. Kama vile haitoshi kwa jinsi Mungu alivyomahiri katika kumfunza mwanadamu kwa vitendo kuwa yeye ni tajiri kwa jinsi alivyomuumba kama atajitambua basi akaleta mifano kama wa ndege mdogo asie na mikono wala pesa anakuwa na uwezo wa kijijiengea makazi yake safi kabisa na ndani ya myumba yake hiyo ndogo akaeka mpaka masponji ili alale kwa raha, mifano ipo mingi. Wadau kama tutakubaliana katika awamu hii ya tano ya Magufuli amekuja kututhibitishia kwa vitendo kuwa watanzania sisi sio masikini na kwa uthubutu wake Tanzania kwa kasi ya ajabu inaanza kupata ushindi kiuchumi na kimaadili kwa wananchi wake ila tuwe wa kweli kabisa katika sekta ambayo haishi katika awamu ya tano ya Magufuli ni sekta ya michezo bado wadau wake wamelala wakisubiri majaliwa ya Mungu ili kupata ushindi. Bado wapo watanzania wadau wa michezo wenye mawazo ya watanzania kuwa ilikuwa haiwezekani Tanzania tukawa na uwezo wa kumiliki Dream liner kwa kipindi hiki. Ambao nawafananisha na wale wadau wa Mpira wa miguu wenye mawazo yakwamba sisi bado na hatupaswi kwenda world cup au Afcon na kujilaumu kufungwa na Cape Verde ni zambi kwani hata kwa viwango vya soka wametuuzidi? Yaani unawasikiliza wadau wanaojiita wataalamu wa mpira wakati mwengine mpaka unataka kutapika. Rank ya FIFA kitu gani? Bila ya kumpiga aliekuzidi kirenki vipi utaipata nafasi ya kujipandisha kirank? Khassan Mwakinyo aliingia ulingoni na muengereza akiwa na ukubwa gani wa rank mbele yake? Ukiangalia kwa undani utaona kuwa vijana wetu hasa wa mpira wa miguu baada ya kuaminishwa kuwaza makubwa na kuyafanyia kazi mawazo hayo kwa vitendo ili kutoka hapa tulipo na kupiga hatua zaidi utaona watu wanaleta siasa. Vijana wetu wa Taifa Stars katika mechi ya Cape Verde walifanya uzembe hadi tukapigwa kipigo cha aibu. Sema cha kujiuliza kwanini wachezaji wetu walicheza kizembe zidi ya Cape Verde? Hilo ndilo suala la kujiuliza na kurekebisha tatizo lakini tusididanganye kwamba timu yetu ilicheza vizuri. Na Kama taifa stars itarejea tena kucheza ule mchezo wake mnaouiita mzuri wakufungwa magoli 3-0 basi itakuwa ni vitu vya kushangaza sana.
ReplyDeleteAly Saleh kwa mtazamo wangu hauko sahihi. Tunahaki ya kulaumu, kiwango kibovu kikosi kibovu.
ReplyDeleteKocha ashauriwe kwa kikosi kile tunapigwa tena na nyumba ni. Aite wenye uzoefu, hao akina Kesi, Ulimwengu na Gadiel tusiwaone keaho
Aly Saleh kwa mtazamo wangu hauko sahihi. Tunahaki ya kulaumu, kiwango kibovu kikosi kibovu.
ReplyDeleteKocha ashauriwe kwa kikosi kile tunapigwa tena na nyumba ni. Aite wenye uzoefu, hao akina Kesi, Ulimwengu na Gadiel tusiwaone keaho