October 2, 2018


Baada ya kuelezwa kusimamishwa kwa ratiba ya mchezo wa Simba dhidi ya African Lyon uliopaswa kuchezwa wikiendi hii, uongozi wa klabu hiyo umesema hakuna tatizo kwa mechi hiyo kupigwa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema hawaoni tatizo kwa mechi hiyo kuchezwa kwani kuna uwekezekano wa ligi kumalizika nje ya muda.

Manara ameeleza kuwa TFF na Bodi ya ligi bado mpaka sasa hawajapeleka barua rasmi kwao inayoeleza kuwa wamesimamisha mchezo huo ambao inaelezwa utapangiwa tarehe nyingine.

Aidha, Manara amewashauri TFF kuangalia namna ratiba inavyokwenda ili kuja kuepuka ligi kutomalizika nje ya muda.

Ofisa huyo amesema huko mbele kuna ratiba nyingine zinakuja ikiwemo Mapinduzi CUP na Michuano ya Kimataifa hivyo ni vema wakaliangalia suala hili kwa jicho la tatu kuweka mambo sawa.

3 COMMENTS:

  1. ww c ndo wa kwanza kuomba mech yako ya tar.27 istishwe kisa mech na yanga, hukuliona hlo bac nashauri na hlo kubaliana nalo 2 kwan ulzaniaje.?

    ReplyDelete
  2. huyu manara sindio yeye alikua wakwanza kuomba mechi yao ya tar 27 na biashara isogezwe mbele kwani hayo anayoyaongea Leo hakuyaona? wacha tu tff wasogeze mbele usitafute visingizio majigambo sasa hakuna kikosi cha bil.3.5 mechi 6 point 11 nafasi ya 9

    ReplyDelete
  3. huyu manara sindio yeye alikua wakwanza kuomba mechi yao ya tar 27 na biashara isogezwe mbele kwani hayo anayoyaongea Leo hakuyaona? wacha tu tff wasogeze mbele usitafute visingizio majigambo sasa hakuna kikosi cha bil.3.5 mechi 6 point 11 nafasi ya 9

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic