October 2, 2018


Hili halikuwepo huko nyuma! Kwamba umkute staa wa kike yuko na baunsa, ilikuwa ni jambo adimu sana, lakini sasa hivi imekuwa fasheni. 

Mbali na mastaa wa kiume kama Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye haendi sehemu bila baunsa, sasa hivi na mastaa wa kike nao wameamua kupita humohumo, kila wawapo hasa usiku, pembeni wanakuwa na wanaume maarufu kama mbavu nene, yaani walinzi.

Kwa sasa mastaa wa kike Bongo ambao wana mabodigadi ni Jacqueline Wolper, Lungi Maulanga, Irene Uwoya, Wema sepetu na wengineo. 

Kinachoelezwa mara nyingi ni kwamba, sababu hasa ya kuongozana na wanaume hao ni usalama wao, kwamba wao kama mastaa wana maadui hivyo endapo litatokea la kutokea au ikitokea vurugu, basi wawe na watu wa kuwasaidia.

“Ndiyo maana baadhi wanapenda washikwe mikono na mabaunsa wao, washikwe kiunoni, mabegani na sehemu nyingine za mwili ili tu wasijihisi wapweke.


“Lakini pia ni ‘show off’ tu! Kuna baadhi ya mastaa wanapenda wanapofika kwenye shughuli wazungumziwe, wawe gumzo, watengeneze habari kwa hiyo watabuni vitu mbalimbali vya kuwapa kiki na ndiyo maana wengine hata bila sababu watakodi wanaume wa kuongozana nao kama mabausa na kujinadi kuwa wanawalipa pesa ndefu, kumbe ni siku hiyo tu.

“Pia kuna mastaa ambao wanavaa nguo ambazo ili wawe huru lazima wawe na watu pembeni, kwa mfano unaweza kukuta staa kavaa nguo fupi sana kiasi kwamba akidondosha kitu kuokota ni mtihani au kavaa gauni refu linalohitaji kushikiliwa, wanaume hao wanafanya kazi hiyo.”

1 COMMENTS:

  1. Makubwa kha! Hao mabaunsa wawe wanaheshimu hiyo kazi yao ya kinda walimbwende wasije wakainanga profeshinal ya watu kwani ubaunsa ni kazi ya zamana. Wakitaka kujifunza zaidi juu ya maadili ya kazi ya ubaunsa basi wazidi kuangalia movie ya Bodyguard ya Whitney Houston,watajifunza mengi. Ila wadada lazima watofautishe kati ya mabaunsa ma wapenzi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic