October 2, 2018


Imeelezwa kuwa Shirikisho la Soka Tanzania kupitia Bodi ya Ligi limesogeza mbele mechi za Simba na Yanga kutokana na wachezaji wake kuitwa katika kikosi cha Taofa Stars.

Taarifa hiyo imekuja ikiwa Simba na Yanga tayari zimeshaanza maandalizi kuelekea mechi zake zijazo za ligi.

Simba walipaswa kucheza na Africal Lyon wikiendi hii lakini sasa itabidi wasicheze kutokana na kuelezwa kusimamishwa mchezo huo ambao utapangiwa tarehe nyingine.

Aidha Yanga nao baada ya kucheza na Simba Jumapili ya wiki jana, tayari walishaanza kujifua kuelekea mechi yao na Mbao ambayo ilipangwa kuchezwa Jumapili ya wiki hii.

Licha ya taarifa hiyo kusambaa, bodi ya ligi mpaka sasa haijatoa tamko lolote la uthibitisho wa kupangua mechi hizo ambazo zilipaswa kuchezwa wikiendi hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic