November 8, 2018


Na George Mganga

Klabu ya Azam FC imemtambulisha rasmi mchezaji wa kimataifa, Mzambia, Obrey Chirwa.

Chirwa amejiunga na Azam baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Nogoom El Mostakbal inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri ambayo alisajiliwa hivi karibuni.

Mshambuliaji huyo ametua Azam akiwa ameshawahi pia kuichezea Yanga na kisha baadaye kukimbilia huko Uarabuni baada ya mambo ya kifedha na mabingwa hao wa kihistoria kutokuwa sawa.

Baada ya kurejea nchini, awali ilielezwa Chirwa angeweza kurudi Yanga lakini mambo yamekwenda tofauti.

Chirwa sasa ataanza rasmi kuitumikia Azam kuanzia Novemba 15 2018 ambapo dirisha dogo la usajili litakuwa limeshafunguliwa.




4 COMMENTS:

  1. Duh! Maskini jirani! Kama huna pesa huwezi kumpata mwanamke mzuri!

    ReplyDelete
  2. Walisema hawawezi kumchukua kwa sababu ni msumbufu. Sasa na atawasumbua sana na beki yao kule Jangwani.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  3. Hawa jamaa (majirani), hawakosagi sababu; Ngoma alipoenda Azam, wakasema acha akawaonyeshe jeuri, jamaa kaenda sasa ana magori matatu na anaendelea kukipiga kama kawa. Na sasa ameenda Chirwa, cjui watawaambiaje Azam! Hamjiulizi jirani zetu, kwanini wachezaji wazuri na makocha wazuri wanawakimbia? lakini wakienda timu zingine wanatulia! TATIZO PESA JIRANI ZETU. Na dirisha dogo hilooo ndo lishakaribia, wengine wameanza visababu kidogo-kidogo; mara hawaji mazoezini, wataanza kugomea kwa kudai mishahara yao, na mengine, timu itapukutika hiyo!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic