November 8, 2018


Uongozi wa timu ya Yanga umewatupia dongo kimtindo timu ya Simba ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo kwa tofauti ya mabao ya kufunga, wakiwa na mabao 23  tofauti ya mabao 6 na Yanga wenye mabao 17  ambapo wote wana pointi 26.

Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa mipango kwa timu inaendelea vizuri na amewatupia dongo kimtindo wapinzani wao Simba ambao wamezidi mchezo mmoja na kuwa sawa kwenye pointi.


"Tunastahili kuitwa mabingwa wa kihistoria kwa kuwa rekodi zetu hazijafikiwa na timu yeyote, msijisahau sana, pointi sawa mmezidi mchezo mmoja," alisema.


Simba wamecheza michezo 11 kwenye ligi huku Yanga wakiwa wamecheza michezo 10 na wana mchezo mmoja mkononi.

16 COMMENTS:

  1. Dismas ten kashaangukaga chooni nn ameshajua yanga imeshakufa ndoo anasema mabingwa wa kihistoria kwenye mpira akuna mabingwa wa kihistoria ulaya ulikotoka ulishasikia kuna timu inaitwa mabingwa kwa kihistoria juve psg wametawala soka la nchini kwao tena kwa kuchukua back to back mara tano mwingine mara sita lakin uyu boya wa yanga anajiita mabingwa kwa kihistoria kwa lipi kwa nn waaijiite mabingwa wa kihistoria wa kuomba omba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana km inauma hayo maneno tu ya mtaani acha ushamba

      Delete
    2. heeh hheh hheh....kama inakuuma chomoa

      Delete
    3. Acha ushamba kila nchi ina bingwa wa kihistoria,bingwa wa kihistoria Uingereza ni Man U,Bingwa wa kihistoria. UEFA ni Real Madrid etc
      Kigumu kuelewa ni nini hapo,bingwa wa kihistoria maana yake aliye kwenye vitabu vya kumbukumbu kuwa aliyetwaa ubingwa mara nyingi kuliko timu zote

      Delete
    4. Historian haifutiki.Dismas katumua historian kuiinua Yanga katika kusudio LA mktadha Wa chapisho lake.Kwani nikweli Yanga ni mapingwa kihistoria ni mabingwa waliopata kuwepo.Use makini anayesema Yanga ni mabingwa Wa kihistoria sio Dismas Ten,bsli ni histotia yenyewe ndiyo imejiandika.Time will tell, maana hata ninyi simba mkijipanga vizuri mkamchapa Zahera misimu mitatu ya ligi mfurulizo mkawa mabingwa.Tutawaita hivyo hivyo.Lkn mkazane sijui kama Mtambwaga Zahera.cocha wa gharama kutoka uzunhuni miezi sits kazini haokoti hata ukocha bora wa mwezi!ngoja tungojee Novemba nafikiri inaweza kumwibua kocha toka bars.pole

      Delete
  2. Daaah, mwandishi naona hapa unatafutiza tu habari, hakuna flow, connection ya dongo na mabingwa wa kihistoria hapo. Jaribu kujenga hoja ya kiongozi wa Yanga Dismas Ten kuwapiga dongo Simba. Mbona hakuna connection ya dongo na ubingwa wa kihistoria?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahaha kweli sijaona dongo hapo kwenye taarifa

      Delete
  3. Kwani Ligi ndo haichezwi tena milele! Historia ni kwa jambo lililokufa au halitatokea tena na kubakisha kumbukumbu tu! Mfano Kombe la Hedex au Jamhuri ya Muungano! Hapo historia sawa! Napita tyuuuuu

    ReplyDelete
  4. Yanga wanatakiwa kujua ubingwa sio wa ligi kuu TPL au VPL kama ilivyokuwa. Kuna ubingwa kombe LA FA, Kagame nk..Ili kuwa ubingwa wa historian wahesabu vikombe vyote walivyonavyo..Yanga sio timu inayoongoza kwa vikombe Tanzania..Wameshaanza kupata safe tena uwanja wa Dar.Next wako Shinyanga na Bukoba..kila LA heri!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga ni bingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania,Simba ni bingwa wa kihistoria wa Hedex Cup,Mapinduzi Cup,Mtani Jembe etc mbona Simple.It will never change,Yanga fought hard for that recognition,Simba waache mdomo wacheze soka labda iko siku bingwa wa kihistoria wa Soka la Tanzania watakuja kuwa wao,lakini kwa sasa ni Dar Young Africans

      Delete
  5. Hoja yangu siyo kama maneno ya mtaani, hii blog inalipwa fedha na imesajiliwa kutoa taarifa za ukweli na uhakika siyo tetesi au maneno ya mtaani. Kumbuka hizi ni kumbukumbu na watu wanatunza siyo vizuri kuandika hisia za mtu na kuwa facts. Haaaaaaa najaribu kuweka sawa hoja ya DOGO JAMANI

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  6. Yote kwa yote, tukirejea maneno ya mlengwa (Ten), anasema wao wanastahili kuitwa mabingwa, sababu yake ya kusema hivyo ni kwa sababu ana mechi moja mkononi, hivyo anapigia mahesabu kama vile ameshaishinda na hiyo mechi, mechi yenyewe ya kiporo anaenda kucheza Kambarage. Yaani jamaa anapigia mahesabu ya kuchukua mahali ya mamilioni kwa mtoto ambaye bado hajamzaa; je akizaliwa dume na mahali ya watu umeshakula na huna uwezo wa kurudisha! au umezaa "bahati mbaya". Jivunie na kile ulichonacho mkononi bwana Ten.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usimlishe maneno hajasema yeye ni bingwa wa kihistoria kwa sababu ana mechi moja mkononi unachangaja madawa,alianza kwa kukumbushia fact kwanza ambayo ndio ukweli wenyewe,Simba mjifunze kuishi na hiyo fact vinginevyo itawatafuna sana mioyo yenu,pambaneni labda siku mtaibadilisha hiyo fact

      Delete
    2. Ivi cku yanga akicheza final ya CAF itakuwaje mbona simba kacheza lakn tumetulia

      Delete
  7. Maudhui ya habari haina muunganiko wa bingwa wa kihistoria, suala la kukumbushana na kushika nafasi ya pili ya Simba hapo ndipo tunapohoji kupambana na ubingwa wa kihistoria, utapambanaje wakati ndo wanavyosema? Hapa muunganiko wa sentensi haupo sawa kiongozi.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  8. Kama yanga ni bingwa wa kihistoria , mtueleze pia bingwa wa kijiografia , kisayansi , ki hisabati , ki fizikia na ki biolojia ni nani. Hao wanaojiita mabingwa wa historia waulize Tanganyika ilipata uhuru wake mwaka gani kama kuna mchezaji hata mmoja atakujibu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic