November 20, 2018


Baada ya kuambulia kichapo cha bao 1-0 juzi katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Lesotho, imeelezwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mnigeria, Emmanuel Amunike, aliwapanga wachezaji pekee waliokuwa wanajituma mazoezini.

Taarifa za ndani kutoka kambi ya Taifa Stars iliyokuwa huko Afrika Kusini kwa takrirani siku zinasema Amunike aliamua kuwapa nafasi wale waliokuwa wanajituma kupiga tizi la maana pekee.

Maamuzi ya Amunike kuwapanga wachezaji hao yaliwafanya wale wazoefu na waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kucheza mchezo huo kupigwa chini na Mnigeria huyo.

Kitendo cha kuwaweka benchi wachezaji kama Shiza Kichuya ambaye japo aliingia kipindi cha pili wakati Stars ikiwa imelala pamoja na John Bocco, Shiza Kichuya, Feisal Salum 'Fei Toto' na wengine kumezua gumzo kubwa kwa mashabiki.

Wachezaji hao waliokuwa wanapewa naafsi kubwa ya kuiangamiza Lesotho imeelezwa Amunike aliamua kuwaweka pembeni baada ya kutoonesha jitihada za kujifua kwenye kambi waliyoweka huko Afrika Kusini.

Stars baada ya kukumbana na kichapo hicho, sasa itawabidi washinde mchezo ujao dhidi ya Uganda huki wakiwaombea Cape Verde kuwamaliza Lesotho.

18 COMMENTS:

  1. Kinachoendelea ndani ya Taifa Stars ni siasa za kipuuzi.Hivyo kwa bosi anaetaka kazi yake kufanywa kwa ufanisi atakabidhi kazi kwa nani kati ya anaeijua na anaetaka kujua? Timu ya Taifa kimsimgi sio mahala kwa wachezaji kwenda kufanya mazoezi kufa,ni mahala pa ufundi zaidi na mbinu za haraka za kuwaunganisha wachezaji kuwa kitu kimoja lakini Taifa Stars katika mechi tatu chini ya Amunike kumekuwa na Taifa Stars tatu tofauti muunganiko huo wa timu utapatikana wapi? Kwa mwendo huu hata Mfanao Taifa Stars ifuzu Afcon basi ni kwenda kupata aibu tu.

    ReplyDelete
  2. Duh ameshaanza visingizio visivyo na tija.Ukweli kocha hakuwa na tactics na hata ukiangalia mechi zote alizoongoza timu yetu ya Taifa ni juhudi za wachezaji binafsi (individual skills) na ukirejea mechi hizo utaona timu yetu haupigi pasi zaidi ya nne na kupoteza mpira kwa adui.Excessive physical training haitajiki kwenye timu za Taifa bali kinachohitajika ni mbinu.Nina wasiwasi na CV ya kocha kuwa ni ya nadharia zaidi ambayo haina uzoefu wa kufundisha timu za Taifa.Bora mechi ya mwisho na waganda mpatieni kocha Kibadeni na akisadiana na Ali Bushiri

    ReplyDelete
  3. Aende tu huyu kocha, hiyo ni sababu ya kumdanganya mtoto "nitakuletea pipi". Hana uwezo wa kufundisha timu kubwa bali huyu kaja kuongeza CV yake tu hapa. Na hii ndio sababu hata hao TFF wakati wanamleta walituficha hata kutuonyesha CV yake. Huwezi ukawajaribu wachezaji kwenye mechi critical kama ile. Na kwanini asingesema mapema kuwa kuna wachezaji kadhaa hawafanyi mazoezi kwa juhudi kwahiyo sitawapanga, kwani kambi si imegharimu siku kumi zote, alishindwa kuliweka hilo bayana? na pia kazi yake ni nini au alichukua jitihada za kuhakikisha uvivu huo wa mazoezi unaachwa na wachezaji hao? Kazi yake ni nini akiwa ndiye kocha? Au kuna mtu mwingine ambaye anahusika na suala la nidhamu ya wachezaji? Kutomchezesha mchezaji muhimu wa Taifa unakuwa unamkomoa nani? na ukizingatia mashindano haya ni ya kuangalia points zaidi ni kama ya mtoano! huwezi kusema kuwa nitarekebisha mechi ijayo! sasa ona mzigo mkubwa ambao ametutwisha huyu jamaa! NA AENDE TU! Hana jipya la kutuambia wala kujitetea. Akafundishe timu za academy huko kwao. Hata uwezo wa kufundisha timu za ligi anaonekana hana.

    ReplyDelete
  4. Kocha gani aliekuja kwetu akawa bora tatizo kwetu sio walimu .hata aje mourinho bado tutamfukuza na kumuona hafai.ule ndio uwezi wetu ambao tumeuanda.kwenye mpira hakuna shortcut

    ReplyDelete
    Replies
    1. No tena big no wakati wa Maximo hatakua na wachezaji wanacheza nje na kocha alifanya kazi na wachezaji wa ndani mpaka

      Delete
  5. Kwa kweli tuangalie hata kama siyo kocha mm ningepanga hivi
    1 Manila
    2 messy
    3 mbaga
    4 Banda
    5 yondani
    6 mkude
    7 kichuya
    8 fei
    9 bocco
    10:chilunda
    11 msuva
    SUB
    Kakolanya
    Agrey
    NYONI
    Mao
    Mudathir
    Farid
    Kimenya
    Mandawa
    Nipeni Lesotho hapo wangekula nyingi tu

    ReplyDelete
  6. Na wewe tungkuzomea , umepnga list nzuri lakini kwa kesi umechemsha afafhali hata ys Nyoni nae kiraks snaweza kuzuia na kupanda akicheza beki za kulia ama kusjoto

    ReplyDelete
  7. Sababu gani za kipuuzi kocha. Hivi tunge kuwa tunapanga makocha wanaojituma hapa nchini kwa kuwezesha timu wanazofundisha, kwangu mimi wewe ungeangukia mkia chini kabisa ya kocha wa Yanga namba 1, anafuatia kocha wa Azam, anafuatia kocha wa Simba. Kiukweli wachezaji ulioacha kuwapanga mapema, hao ndio wangetuvusha. Unampanga striker bora dakika 9 mpira kwisha? Lakini pia kwanini ushindwe kuwa na mahusiano mazuri na wachezaji wako wote? wewe ndio mwalimu unashindwa kutengeneza mahusiano mazuri kila mara wachezaji hawana raha why? Tutoke huko.

    ReplyDelete
  8. Maamuzi ya kitoto aliyo yafanya , kwa mtazamo wangu uyo kocha hatutakii mema, tunaipenda timu yetu na ushindi wao ndo furaha yetu ka hawezi soka la bongo aende zake kwao lags

    ReplyDelete
  9. Kufundisha timu ya Taifa ni tofauti na kufundisha klabu na tofauti na kufundisha timu ya taifa ya vijana

    Kwenye timu ya vijana unaweza kuwa nao kambini hata kwa siku thelathini, kwa kuwa wao ni vijana utawafundisha vitu vingi sana hata , utakuwa na muda wa kumbadilisha namba mchezaji wa kati na kumfanya awe winga mzuri, utaweza kumbadilisha kiungo wa kati awe beki wa kati n.k...

    Ukifundisha klabu utakuwa una muda mwingi wa kufanya mazoezi na wachezaji wako hata mara tatu kwa siku, utakuwa na muda wa kutengeneza 'combination' ya wachezaji, utaweza kuwabadilisha nafasi walizozizoea na kuwachezesha nafasi tofauti , utazingatia wachezaji wanaojituma zaidi ndio wacheze mechi , utawafundisha jinsi ya kupiga krosi,faulo, kukaba nafasi n.k , pia kwa kuwa una muda mwingi

    Katika timu ya Taifa ya wakubwa muda wa kufanya mazoezi huwa ni siku tatu tu, hapo walimu hawafundishi vitu kipya bali mbinu na vipaji kwa kuwa hakuna muda wa kutosha

    ReplyDelete
  10. Kufundisha timu ya Taifa ni tofauti na kufundisha klabu na tofauti na kufundisha timu ya taifa ya vijana

    Kwenye timu ya vijana unaweza kuwa nao kambini hata kwa siku thelathini, kwa kuwa wao ni vijana utawafundisha vitu vingi sana hata , utakuwa na muda wa kumbadilisha namba mchezaji wa kati na kumfanya awe winga mzuri, utaweza kumbadilisha kiungo wa kati awe beki wa kati n.k...

    Ukifundisha klabu utakuwa una muda mwingi wa kufanya mazoezi na wachezaji wako hata mara tatu kwa siku, utakuwa na muda wa kutengeneza 'combination' ya wachezaji, utaweza kuwabadilisha nafasi walizozizoea na kuwachezesha nafasi tofauti , utazingatia wachezaji wanaojituma zaidi ndio wacheze mechi , utawafundisha jinsi ya kupiga krosi,faulo, kukaba nafasi n.k , pia kwa kuwa una muda mwingi

    Katika timu ya Taifa ya wakubwa muda wa kufanya mazoezi huwa ni siku tatu tu, hapo walimu hawafundishi vitu kipya bali mbinu na utazingatia vipaji kwa kuwa hakuna muda wa kutosha

    ReplyDelete
  11. Huyo kocha hafai. Tulimpapatikia kwa kuwa alicheza Barcelona. Hajawahi kufundisha timu yoyote kubwa. Alifundisha timu fulani ya Uarabuni isiyojulikana. Atuachie Taifa Stars yetu asepe. Kocha gani hajui kuchagua wachezaji wala hajui kuusoma mchezo? Hafai hafai hafai!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic