November 20, 2018


Mwenyekiti wa timu ya Simba kwa upande wa klabu, Sued Mkwabi amesema kuwa wamejipanga kuweza kuleta ushindani kimataifa ili kuweza kuwapa raha mashabiki wao.

Simba wanawakilisha taifa katika mashindano ya Ligi ya klabu Bingwa Afrika, ambapo mchezo wao wa kwanza utakuwa Novemba 28 dhidi ya timu ya Mbabane Swallows FC ya Swaziland.


"Tumejipanga kiasi cha kutosha kuweza kupata matokeo mazuri mbele ya wapinzani wetu na tunatambua kwamba masahabiki wanahitaji matokeo hicho ndicho tutakachofanya.


"Kocha Mkuu, Patrick Aussems anasuka kikosi cha ushindi ambacho kitaleta ushindani, kikubwa ni mashabiki wawe bega kwa bega nasi katika kufukuzia mafanikio, nina imani tutafika mbali," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic