November 20, 2018


Aliyekuwa kuwa Kocha wa Gor MahiaFC  ya Kenya, Dylan Kerr, ametangazwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Black Leopards inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika kusini.

Kerr amemalizana na klabu hiyo ambayo inashiriki ligi ya nchini humo ambayo mtanzania Abdi Banda anacheza pia kwenye timu ya Baroka FC.

Kocha huyo kutokea England alieleza kuachana na Gor Mahia kutokana na kupata dili hilo baada ya kuelewana na mabosi wake kisha kuelekea zake Afrika Kusini.

Muingereza huyo atatambulishwa rasmi siku yoyote kuanzia leo ndani ya klabu hiyo iliyo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi huku ikiwa imecheza mechi 11.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic