November 21, 2018

Uongozi wa timu ya Azam FC, umesema kuwa hatma ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima na Kiungo mkabaji wa Yanga Papy Tshishimbi upo mikononi mwa kocha mkuu Hans Pluijm.

Niyonzima na Tshishimbi wamekuwa wakihusishwa kujiunga na Azam FC kwenye dirisha dogo lilifunguliwa Novemba 15 huku Azam wakiwa wameshamsajili Obrey Chirwa kwa kandarasi ya mwaka mmoja.


Ofisa habari wa Azam FC, Jaffari Maganga amesema kuwa suala la wao kufanya usajili hilo lipo wazi ni lazima waboreshe kikosi chao kutokana na ushindani uliopo.


"Pluijm ndiye mwenye maamuzi ya mwisho juu ya wachezaji hao, tunatambua kwamba wana mikataba na timu zao, tutafanya kazi kwa kuzingatia utaratibu kama kutakuwa na uhitaji wa kuwasajili tutafanya hivyo.


"Kwa sasa hatuna mazungumzo nao kwa kocha hajasema kama anawahitaji tunaangalia namna ya kuweza kuwa bora zaidi ya msimu uliopita," alisema.  

4 COMMENTS:

  1. Niyonzima ha ha ha ha mbona mtasugua sana hamuwezi mchukua yule hata mfanye nini simba ina pesa wewe kama ndio mnalojivunia hapo mmebugi axeee.

    ReplyDelete
  2. Jina lililopo free ni giyani kama mnalihitaji chukueni chap,ila kwa niyonzima ha ha ha ha narudia tena imekula kwenu huyo ni mali ya simba ndugu zangu.

    ReplyDelete
  3. Jina lililopo free ni giyani kama mnalihitaji chukueni chap,ila kwa niyonzima ha ha ha ha narudia tena imekula kwenu huyo ni mali ya simba ndugu zangu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic