November 21, 2018


Ofisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara amesema wamejipanga kuweza kufuta rekodi iliyowekwa na Lipuli FC msimu uliopita kwa kutoka nao sare michezo yote miwili.

Manara amesema walishindwa kupata ushindi mbele ya Lipuli FC ambayo ipo chini ya kocha Seleman Matola kutokana na uzoefu wa Kocha.


"Tulipata taabu sana kwa Lipuli msimu uliopita, kwa sasa tumejiandaa ili kuweza kuvunja rekodi hiyo hasa kutokana na kikosi chetu kuimarika," alisema.


Simba watacheza na Lipuli Ijumaa katika uwanja wa Taifa Dar es salaam, majira ya saa kumi kamili.

1 COMMENTS:

  1. Labda kama ma proo fessionals hawapo ndio LIPULI watapata japo suluhu,but kama majembe yapo mbona shuhuli wanayo hao tena sio chini ya mbili.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic